TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 30 September 2010

Mbatia kujenga gati Kawe

Na Peter Mwenda
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia amewaahidi wakazi wa
jimbo la kawe kuwa akichaguliwa kuwa
mbunge atajenga gati (bandari ndogo) itakalosaidia kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni Kata ya Tegeta juzi Bw. Mbatia alisema foleni na misongamano ya magari jijini Dar es Salaam inachangia kupunguza uzalishaji na kusababisha Serikali kupoteza sh. Bil 4 kwa siku.
Alisema kuna njia nyingi ya kuondoa msongamano huo lakini katika jimbo lake anaweza kujenga gati ya kushushia na kupandisha abiria litakalogharimu sh. bil. moja ambazo ni sawa na thamani ya magari mawili yanayotumiwa na Rais, Jakaya Kikwete.
"Fedha zinazopotea kutokana na wananchi kutumia muda mwingi barabarani unapoteza sh. bil. 4 ambazo zinatosha kununulia madawati 80,000 kwa siku" alisema Bw. Mbatia akionesha kuwa na uhakika wa utafiti wa takwimu hizo.
Alisema Serikali imeshindwa kuwatumia wataalamu wake akiwemo yeye ambaye ni mtaalamu wa ujenzi wa bandari aliupata nchini Uholanzi na sasa anataka kuutumia kuondoa kero za wananchi wa Jimbo la Kawe watumie usafiri wa majini kufika katikati ya Jiji.
"Nashangaa kusikia inajengwa bandari nyingine Bagamoyo badala ya kuiboresha iliyopo ya Dar es Salaam ambayo haiko katika idadi ya bandari 500 zinazofahamika duniani"alisema Bw. Mbatia.
Alisema asilimia 98 duniani husafiri kutumia vyombo vya majini lakini katika jiji la Dar es Salaam uwezo wa kujenga gati la kusafirisha abiria asilimia 30 wanaoteseka kwa foleni utapunguza msongamano wa usafiri na kuongeza uzalishaji.
Bw. Mbatia alisema utaratibu wa kimataifa ni kuwa bomba la maji machafu linaloingia bandarini linatakiwa kufanyiwa marekebisho ili maji machafu hayo yachujwe kwanza ndipo yaingizwe baharini badala ya kupeleka moja kwa moja.
Alisema fani yake ya uinjinia anashindwa kuitumia Tanzania kwa sababu hapewi ushirikiano lakini nchini Uholanzi wanathamini mchango wake kwa sababu anapewa mkataba wa kufundisha Chuo Kikuu nchini humo.
Alisema amejipanga kuleta maendeleo ya kweli katika Jimbo la Kawe ambayo hayajawahi kufanywa na wabunge waliopita na kutumia nafasi yake kuibana Serikali iwaondolee wananchi wa Kawe kero mbalimbali za Maji, Miundombinu,soko la kisasa na mengine.
\


Tuesday, 28 September 2010

Kila Ijumaa na Jumamosi ni pale Sanaa Pub, usikose mdau....!

Every Fridays and Saturdays at Sanaa Pub Movenpick.

Times Fm Djz...

Dj Spesso,Dj Kobbo Lil Ommy.
Naija,Kwaito,Ragger,Bongo,Hip&Rnb,Pop,Old School and More.

Entry-5000/=

Come One Come All Yaa!

Monday, 27 September 2010

DC Gama awatoa hofu wanaodai fidia Kigilagila

Na Peter Mwenda MKUU wa wilaya ya Ilala, Bw. Leonadis Gama amewataka wakazi wa Kigilagila wanaosubiri kuhamishwa kupisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dares Salaam (DIA)watulie wakati maandalizi ya kufufua viwanja,ujenzi wa barabara unafanyika.
Akizungumza na majira ofisini kwake jana. Bw. Gama alisema msimamo wa Serikali upo pale pale kuwa inandaa viwanja na kuweka barabara ili malipo ya fidia yakianza wapewe na ofa za viwanja vyao.
"Hatuwezi kurudia makosa ya Kipawa,tunataka mtu akilipwa fidia anapewa ofa yake ya kiwanja,hatutakwenda kinyume wanatakiwa kuwa watulivu" alisema DC Gama.
Aliwatahadharisha wananchi kuacha kununua viwanja kiholela kwa kuamini wenyeji na wajumbe wa mashina bila kufuata taratibu zinazohusika za manunuzi ya ardhi kwa sababu maeneo mengi yanayouzwa yamenunuliwa na Serikali.
"Watu wengi wanaingizwa mkenge kuuziwa maeneo ambayo yamenunuliwa na Serikali kwa kusimamiwa na mjumbe wa shina anayetoa hati ya mauzo, pateni uhakika wa maeneo hayo katika Manispaa kujua eneo hilo ni nani miliki halali" alisema DC Gama.
Alisema viongozi wa Serikali za mitaa, watendaji na viongozi wa Kata waweke mikakati ya kulinda uharibufu wa afrdhi unaofanywa na baadhi ya watu wenye tamaa ya kuchimba mchanga bila kuwa na vibali.
Bw. Gama alisema tatizo na uvamizi wa ardhi ni sugu katika jiji la Dar es Salaam amewataka wananchi wabadilike kujiepusha kujiingiza katika migogoro isiyo ya lazima.
Wakazi wa Kigilagila walilalamika hivi karibuni kuwa awali walitarifiwa fidia zao kuanza kulipwa kutoka Mei mwaka huu lakini mpaka sasa hajaelezwa sababu ya kutolipwa.
Walidai kuwa kutoka wathaminiwe nyumba zao mwaka 1997 pamoja na Kipawa hatujaziendeleza nyingine zimebomoka huku wakisubiri kulipwa fidia bila mafanikio.
Mwanasheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege,Bw. Ramadhani Maleta alipohojiwa wiki iliyopita alitoajibu kama hilo kuwa watalipwa siku chache zijazo baada ya kukamilika kazi ya kupima viwanja na kuchonga barabara za mitaa.

Thursday, 23 September 2010

Peter Mwenda (Buyoya) atimiza miaka 50 (Nusu Karne)

MIMI ni mzaliwa wa kijiji cha Masange wilaya ya Kondoa kabila langu Mrangi ni baba wa watoto watano wa kiume na mke mmoja Elizabert John Mwenda (40) kutoka mkoa wa Mbeya.

Nilifunga ndoa na mke wangu mwaka 1992 katika Kanisa Katoliki Parokia ya St. Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati huo tukiwa na watoto wawili Joseph (Tiria) na John.

Naishi Kitunda, Kivule wilaya ya Ilala nikifanya kazi ya uandishi kampuni ya Business Times katika gazeti la Majira.

Ni muumini wa kanisa Katoliki ambako mwaka huu nilichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Utume Wanaume Katoliki (UWAKA) katika Parokia  Mpya ya Kitunda.

Nimepita katika vikwazo vingi vya maisha ikiwemo kuumwa kwa zaidi ya miaka mitatu nikisumbuliwa na magonjwa mbalimbali (siyo UKIMWI) namshukuru Mungu kunivusha katika mitihani hiyo sasa nimepona.

Kilikuwa kipindi kugumu kwa familia, ndugu, majirani, waandishi wenzangu wengine waliniombea nipone, wengine walikata tamaa kwa hali niliyokuwa nayo na wengine walikaa kusubiri kusikia simu ikipigwa kuwapa taarifa ya kifo na wengine kunitangaza nimeathirika.

Wote hao nina wapenda kwa sababu kila unapoishi usifikiri kila mmoja anao upendo wa dhati na wewe,ishi ukijua kuwa nafsi yako ndiyo itakuokoa mbele ya Mungu na wasamehe wote waliokukosea.

MUNGU NINYOSHEE MKONO WA BARAKA NIENDELEE KUWATUMIKIA KWA DHATI WATANZANIA WENZANGU KUWAHABARISHA YALIYO YA KWELI TU!

Amina!

Wednesday, 22 September 2010

ZAIN YAPUNGUZA GHARAMA ZA UPIGAJI SIMU 50%


  Kampuni ya simu za mkononi ya Zain, imetangaza punguzo la gharama za simu kwa wateja wake kwenda mitandao mingine kwa asilimia hamsini.
  Kuanzia sasa, wateja wa Zain watapiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama ya sh 3 kwa sekunde siku nzima.
  Punguzo hili ni muendelezo wa mkakati wa Zain wa kutoza viwango nafuu baada ya kuanzisha sh 1 miezi michache iliyopita.
  Akizungumza na waandishi wa habari Dar-es-salaam leo, Sam Elangalloor, Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania amesema, “Tunajivunia zaidi kwa kuwa mtandao nafuu hapa nchini kuliko mtandao mwingine wowote na katika kuthibitisha hilo, leo tena tumeweza kushusha gharama mpaka nusu ya gharama za mwanzo.
  Tunaamini kila mtanzania ana haki ya kuwasiliana na zaidi ya wateja wetu milioni 5 watafurahia punguzo hili la asilimia 50. Zaidi ya hayo, wateja wa Zain wataweza kupata sms 4 za bure kwenda mitandao mingine yeyote.
  “Wateja wote wa malipo ya kabla na baada watanufaika na punguzo hili. Pia mtakumbuka ya kwamba ni hivi karibuni tu pia tulitoa punguzo za gharama za intanet na za modem hivyo kuwezesha watu wengi zaidi kuwasiliana bila upinzani”, aliongeza Elangalloor.

Muganyizi Mutta


Meneja wa Mawasiliano ya Umma wa Zain Tanzania


0786 670 711

Ushabiki wa kisiasa kama huu wa NCCR-Mageuzi na CCM unaashiria ugomvi

Baada ya CCM kupata habari NCCR Mageuzi na mgopmbea wao wa Jimbo la Kawe, Bw. James Mbatia wanafanya mkutano katika kijiji cha Mabwepande, ilifanya kila jitihada za kukusanya mashabiki wake na kuwafuata huko huko kama inavyoonekana pichani (Picha na Peter Mwenda) Bunju B.

Sunday, 12 September 2010

Mtoto Omari Selemani (10) hajaonekana kwao Kivule siku 25 sasa


Mwanafunzi wa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Kitunda, Ilala Dar es Slaam hajaonekana nyumbani kwao kutoka Septemba 22 alipotumwa na mama yake kununua vitafunio anyee chai aende shule, lakini hajaonekana hata baada ya jitihada za kumtafuta hospitali, vituo vya polisi na ndugu zake  mwenye taarifa awasiliane kwa namba 0715 222677 au baba yake Selemani Omari 0718 507824, 0717 758941 na 0653 589650

Peter Joseph Mwenda anatimiza miaka 50 hivi karibuni

Historia ya Mwenda,maisha yake na familia yake itaanza kuonekana katika blog hii
Gari la polisi linaweza kuimarisha doria Tanzania kupambana na majambazi au kusindikiza msafara wa viongozi?

Mbio za marathon zina raha yake zianzishwe Tanzania

Mbio ndefu hazichagui umri kama inayoonekana pichani

Thursday, 9 September 2010

Zain nayo yafuturisha watoto yatima kabla ya mwezi kuandama Sikukuu ya Eid el Fitri

Kikwete atoa zawadi ya Eid el Fitri

Na Peter Mwenda, Ikulu

RAIS Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya mbuzi,mchele na mafuta ya kusherekea Sikukuu ya Eid El Fitri kwa vikundi kumi vya walemavu, watoto yatima na wazee vyenye thamani ya sh. mil. 4.5

Kaimu Mnikulu, Bw. Kassim Mtawa alisema Rais Kikwete amekuwa akitoa zawadi hiyo kila mwaka na amewatakia watanzania sherehe njema.

Vikundi hivyo ni Kituo cha kulelea watoto yatima cha Sebuleni Zanzibar,Kituo cha kulelea wazee cha Istikama Pemba na Kituo cha Walemavu na Wasiojiweza cha Nunge, Kigamboni.

Kituo cha Watoto Yatima cha RQAM, Dar es Salaam, Kituo cha watoto yatima cha Furaha, Mburahati, Chuo cha Ufundi cha wenye ulemavu Yombo,Kituo cha watoto wenye shida Kurasini,, Kituo cha watoto yatima cha Moyo Mmoja cha Bagamoyo na Kituo cha Yatima Group cha Dar es Salaam.

Pia kipo Kituo cha kulelea watoto yatima cha Child in the Sun cha Kimara ambacho kinasimamiwa na Shirika la Masister Mabinti wa Maria Imaculata chaBarani Afrika wanaosimia Chuo cha St. Joseph cha Mbezi.

Wednesday, 8 September 2010

Jukumu la kusaidia yatima ni langu na wewe, Je mtaani kwako unawasadiaje?

Sister Vasantha Lilly wa Shirika la Masister Mabinti wa Mary Imaculata la Afrika (DMI) akiwa na baadhi ya watoto yatima wa mkoani Ruvuma ambao wanalelewa na masister hao,Shirika hilo lilianzishwa nchini India mwaka 1984..

Karata za wagombea Urais wa CHADEMA, CUF na CCM zaendelea kuchangwa tena

BAADA ya mapumziko ya siku mbili kupisha mtihani wa Darasa la Saba nchini kampeni za kutafuta kura zimeendelea ambako, Dkt. Willibrod Slaa wa CHADEMA akijinadi mkoa wa Singida, Profesa Lipumba wa CUF mkoa wa Lindi na Rais Jakaya Kikwete wa CCM mkoa wa Morogoro.

Matukio-Watu 17 washikiliwa kwa kokota mitihani,picha za Rais Kikwete zachanwa Arusha.

Tuesday, 7 September 2010

Masister mabinti wa Shirika la Maria Imaculata (DMI) linavyosaidia akinamama,watoto yatima Tanzania

Sister Vasantha Lilly (kulia) wa Shirika la Masister Mabinti wa Maria Imaculata wa Kanisa Katoliki Barani Africa (DMI) akishiriki katika maandamano ya akinamama wa mjini Songea katika sherehe ya wanawake nchini.Shirika la DMI limekuwa likisaidia miradi na mikopo ya ujasiriamali kwa wanawake, kulea watoto yatima,

Monday, 6 September 2010

Tendwa awatwanga Chadema K.O

Monday, September 6, 2010

JOHN TENDWA; MKIONA MTU ANALIA MJUE MAMBO SI MAZURI, MKIONA ANACHEKA MJUE MAMBO YAKE POA!!


Msajili wa vyama vya siasa  nchini Bw. John Tendwa amesema hana taarifa yoyote ya kutoa kuhusiana na pingamizi la CHADEMA dhidi ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Katika madai ya Chadema ni kuwa Rais  Jakaya Mrisho Kikwete ameongeza mishahara ya wafanyakazi bila kuhusisha Bunge kitu ambacho kinaenda kinyume na sheria ya Gharama ya Uchaguzi.

Bw. Tendwa ambaye ameahidi kutoa taarifa baada ya siku tano hata hivyo leo waandishi wa habari walipokwenda ofisini kwake kwa ajili kujua hatma ya suala hilo alisema leo ana mkutano mwingine na kuhusu pingamizi la CHADEMA tayari ameshavijibu vyama na pia taarifa ipo Tume ya Uchaguzi ya Taifa .

Hivyo akashauri waende kwa vyama husika na kuwauliza "nendeni kwa wahusika mkawaulize mkiona mtu analia basi mjue mambo yake si mazuri lakini mkiona mtu anafurahia basi mjue mambo yake poa" 

Alhaji Dkt. Maneno Tamba akivuturisha yatima nyumbani kwake Mburahati

Alhaji Dkt. Maneno Tamba (mwenye bargashia) ambaye ni Mganga wa Tiba Asili Tanzania (CHAWATIATA) na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam akigawa vutari kwa watoto yatima wa Magomeni hafla iliyofanyika nyumbani kwake Mburahati jana.

Sunday, 5 September 2010

Akinamama wakipumzika muda mfupi baada ya kufuturu nyumbani kwa Dkt. Tamba alipowafuturisha watoto yatima ambayo huifanya kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani (kulia) ni Mama Tamba.

Padre Babtist Mapunda awaasa wakristo kuchague kiongozi bora si chama

Wakati siku za kupiga kura Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, kumchagua Diwani wa Kata yako, Mbunge wa Jimbo lako na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikijongea, viongozi wa dini mbalimbali Mashekhe, Mapadre, Maaskofu na Machungaji wanahubiri kuchagua viongozi waadilifu.

Padre Baptist Mapunda wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam amewataka wakristo kumpigia kura ndiyo kiongozi atakayekuwa tayari kubadilisha maisha ya watanzania na kuondolea maisha duni, bila kujali anatoka chama gani kati ya 18 vilivyopo nchini.

Friday, 3 September 2010

K I B O N Z O

WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA POOL WAINGIA KAMBINI POOL TABLE VILLAGE

Mkurugenzi mtendaji wa uwanja wa pool table village, Mponjoli Mwakabana (kulia) akiwakaribisha wachezaji wa mchezo huo katika uwanja wake uliopo tandika davis kona jana wakati timu hiyo ilipoweka kambi

TASWA yajitambulisha Wizarani, TFF

Mwenyekiti wa TASWA  Juma Pinto (katikati), Makamu Mwenyekiti Maulid Kitenge, Katibu Mkuu Amir Mhando (Mgosi) kulia.

UJUMBE wa viongozi wa Taswa umekutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Leonard Thadeo na Naibu Mkurugenzi wake Juliana Yassoda.

Taswa ikiwa na Mwenyekiti Juma Pinto, Katibu Mkuu Amir Mhando, Mhazini Sultani Sikilo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Alfred Lucas, walimueleza Mkurugenzi juu ya mipango ya muda mfupi kufikia Machi mwakani ya kuleta mabadiliko kwenye sekta ya michezo na uandishi wa habari.

Kati ya mambo hayo ni Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka, imebadilika ambako na sasa itakuwa kubwa na ya kuvutia hukuwakiomba Serikali iiunge mkono Taswa ili tuzo hiyo ambayo imepangwa kufanyika Februari mwakani ifanikiwe jambo ambalo Mkurugenzi alikubali na kuahidi kutoa msaada kwa kadri atakavyoweza.

Taswa ilimjulisha kuhusiana na mipango ya kuandaa mafunzo kwa wanachama wake ya mara kwa mara ili kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali ya kitaaluma na kimichezo na katika hili pia Mkurugenzi aliliunga mkono na kuahidi kutia nguvu zake kadri awezavyo.

Alishauri uongozi mpya wa Taswa uhakikishe mafunzo hayo yanafanyika vizuri na isiwe kwa kulipua, yawe yale yenye kuleta tija ya uhakika na hilo litafanikiwa kama Taswa itafanya tathmini kabla ya kuendesha mafunzo hayo.

Taswa pia ilizungumzia namna waandishi wanavyokaa uwanjani katika michezo mbalimbali ya soka kwamba hilo huwa linaleta usumbufu, na Mkurugenzi alilichukua na kufafanua kuwa jambo hilo limekuwa pia likijitokeza kwenye vikao vyao mbalimbali, hivyo watalifanyia kazi.

Pia Taswa iliwahi kukukutana na viongozi wa TFF, Makamu wa Kwanza wa Rais Athumani Nyamlani, Kayuni na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Eliud Mvella na Muhsin Said, nao Taswa ikiwakilishwa na Mwenyekiti Pinto, Makamu Mwenyekiti Maulid Kitenge na Katibu Mkuu, Mhando.Thursday, 2 September 2010

Dkt. Slaa akitoa sera za CHADEMA kwa wananchi wa Kiteto katika mkutano ya hadhara
Huyu ni Dkt. Willibrod Slaa mgombea Urais kupitia CHADEMA
Hii ndiyo ngoma ya wananchi wa mkoa wa Dodoma (Wagogo) katika moja sherehe za kampeni za wagombea Urais Tanzania.