TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday 9 September 2010

Kikwete atoa zawadi ya Eid el Fitri

Na Peter Mwenda, Ikulu

RAIS Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya mbuzi,mchele na mafuta ya kusherekea Sikukuu ya Eid El Fitri kwa vikundi kumi vya walemavu, watoto yatima na wazee vyenye thamani ya sh. mil. 4.5

Kaimu Mnikulu, Bw. Kassim Mtawa alisema Rais Kikwete amekuwa akitoa zawadi hiyo kila mwaka na amewatakia watanzania sherehe njema.

Vikundi hivyo ni Kituo cha kulelea watoto yatima cha Sebuleni Zanzibar,Kituo cha kulelea wazee cha Istikama Pemba na Kituo cha Walemavu na Wasiojiweza cha Nunge, Kigamboni.

Kituo cha Watoto Yatima cha RQAM, Dar es Salaam, Kituo cha watoto yatima cha Furaha, Mburahati, Chuo cha Ufundi cha wenye ulemavu Yombo,Kituo cha watoto wenye shida Kurasini,, Kituo cha watoto yatima cha Moyo Mmoja cha Bagamoyo na Kituo cha Yatima Group cha Dar es Salaam.

Pia kipo Kituo cha kulelea watoto yatima cha Child in the Sun cha Kimara ambacho kinasimamiwa na Shirika la Masister Mabinti wa Maria Imaculata chaBarani Afrika wanaosimia Chuo cha St. Joseph cha Mbezi.

No comments:

Post a Comment