MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia amewaahidi wakazi wa
jimbo la kawe kuwa akichaguliwa kuwa
mbunge atajenga gati (bandari ndogo) itakalosaidia kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
jimbo la kawe kuwa akichaguliwa kuwa
mbunge atajenga gati (bandari ndogo) itakalosaidia kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni Kata ya Tegeta juzi Bw. Mbatia alisema foleni na misongamano ya magari jijini Dar es Salaam inachangia kupunguza uzalishaji na kusababisha Serikali kupoteza sh. Bil 4 kwa siku.
Alisema kuna njia nyingi ya kuondoa msongamano huo lakini katika jimbo lake anaweza kujenga gati ya kushushia na kupandisha abiria litakalogharimu sh. bil. moja ambazo ni sawa na thamani ya magari mawili yanayotumiwa na Rais, Jakaya Kikwete.
"Fedha zinazopotea kutokana na wananchi kutumia muda mwingi barabarani unapoteza sh. bil. 4 ambazo zinatosha kununulia madawati 80,000 kwa siku" alisema Bw. Mbatia akionesha kuwa na uhakika wa utafiti wa takwimu hizo.
Alisema Serikali imeshindwa kuwatumia wataalamu wake akiwemo yeye ambaye ni mtaalamu wa ujenzi wa bandari aliupata nchini Uholanzi na sasa anataka kuutumia kuondoa kero za wananchi wa Jimbo la Kawe watumie usafiri wa majini kufika katikati ya Jiji.
"Nashangaa kusikia inajengwa bandari nyingine Bagamoyo badala ya kuiboresha iliyopo ya Dar es Salaam ambayo haiko katika idadi ya bandari 500 zinazofahamika duniani"alisema Bw. Mbatia.
Alisema asilimia 98 duniani husafiri kutumia vyombo vya majini lakini katika jiji la Dar es Salaam uwezo wa kujenga gati la kusafirisha abiria asilimia 30 wanaoteseka kwa foleni utapunguza msongamano wa usafiri na kuongeza uzalishaji.
Bw. Mbatia alisema utaratibu wa kimataifa ni kuwa bomba la maji machafu linaloingia bandarini linatakiwa kufanyiwa marekebisho ili maji machafu hayo yachujwe kwanza ndipo yaingizwe baharini badala ya kupeleka moja kwa moja.
Alisema fani yake ya uinjinia anashindwa kuitumia Tanzania kwa sababu hapewi ushirikiano lakini nchini Uholanzi wanathamini mchango wake kwa sababu anapewa mkataba wa kufundisha Chuo Kikuu nchini humo.
Alisema amejipanga kuleta maendeleo ya kweli katika Jimbo la Kawe ambayo hayajawahi kufanywa na wabunge waliopita na kutumia nafasi yake kuibana Serikali iwaondolee wananchi wa Kawe kero mbalimbali za Maji, Miundombinu,soko la kisasa na mengine.
\
No comments:
Post a Comment