TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 3 September 2010

TASWA yajitambulisha Wizarani, TFF

Mwenyekiti wa TASWA  Juma Pinto (katikati), Makamu Mwenyekiti Maulid Kitenge, Katibu Mkuu Amir Mhando (Mgosi) kulia.

UJUMBE wa viongozi wa Taswa umekutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Leonard Thadeo na Naibu Mkurugenzi wake Juliana Yassoda.

Taswa ikiwa na Mwenyekiti Juma Pinto, Katibu Mkuu Amir Mhando, Mhazini Sultani Sikilo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Alfred Lucas, walimueleza Mkurugenzi juu ya mipango ya muda mfupi kufikia Machi mwakani ya kuleta mabadiliko kwenye sekta ya michezo na uandishi wa habari.

Kati ya mambo hayo ni Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka, imebadilika ambako na sasa itakuwa kubwa na ya kuvutia hukuwakiomba Serikali iiunge mkono Taswa ili tuzo hiyo ambayo imepangwa kufanyika Februari mwakani ifanikiwe jambo ambalo Mkurugenzi alikubali na kuahidi kutoa msaada kwa kadri atakavyoweza.

Taswa ilimjulisha kuhusiana na mipango ya kuandaa mafunzo kwa wanachama wake ya mara kwa mara ili kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali ya kitaaluma na kimichezo na katika hili pia Mkurugenzi aliliunga mkono na kuahidi kutia nguvu zake kadri awezavyo.

Alishauri uongozi mpya wa Taswa uhakikishe mafunzo hayo yanafanyika vizuri na isiwe kwa kulipua, yawe yale yenye kuleta tija ya uhakika na hilo litafanikiwa kama Taswa itafanya tathmini kabla ya kuendesha mafunzo hayo.

Taswa pia ilizungumzia namna waandishi wanavyokaa uwanjani katika michezo mbalimbali ya soka kwamba hilo huwa linaleta usumbufu, na Mkurugenzi alilichukua na kufafanua kuwa jambo hilo limekuwa pia likijitokeza kwenye vikao vyao mbalimbali, hivyo watalifanyia kazi.

Pia Taswa iliwahi kukukutana na viongozi wa TFF, Makamu wa Kwanza wa Rais Athumani Nyamlani, Kayuni na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Eliud Mvella na Muhsin Said, nao Taswa ikiwakilishwa na Mwenyekiti Pinto, Makamu Mwenyekiti Maulid Kitenge na Katibu Mkuu, Mhando.



No comments:

Post a Comment