TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday 27 September 2010

DC Gama awatoa hofu wanaodai fidia Kigilagila

Na Peter Mwenda MKUU wa wilaya ya Ilala, Bw. Leonadis Gama amewataka wakazi wa Kigilagila wanaosubiri kuhamishwa kupisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dares Salaam (DIA)watulie wakati maandalizi ya kufufua viwanja,ujenzi wa barabara unafanyika.
Akizungumza na majira ofisini kwake jana. Bw. Gama alisema msimamo wa Serikali upo pale pale kuwa inandaa viwanja na kuweka barabara ili malipo ya fidia yakianza wapewe na ofa za viwanja vyao.
"Hatuwezi kurudia makosa ya Kipawa,tunataka mtu akilipwa fidia anapewa ofa yake ya kiwanja,hatutakwenda kinyume wanatakiwa kuwa watulivu" alisema DC Gama.
Aliwatahadharisha wananchi kuacha kununua viwanja kiholela kwa kuamini wenyeji na wajumbe wa mashina bila kufuata taratibu zinazohusika za manunuzi ya ardhi kwa sababu maeneo mengi yanayouzwa yamenunuliwa na Serikali.
"Watu wengi wanaingizwa mkenge kuuziwa maeneo ambayo yamenunuliwa na Serikali kwa kusimamiwa na mjumbe wa shina anayetoa hati ya mauzo, pateni uhakika wa maeneo hayo katika Manispaa kujua eneo hilo ni nani miliki halali" alisema DC Gama.
Alisema viongozi wa Serikali za mitaa, watendaji na viongozi wa Kata waweke mikakati ya kulinda uharibufu wa afrdhi unaofanywa na baadhi ya watu wenye tamaa ya kuchimba mchanga bila kuwa na vibali.
Bw. Gama alisema tatizo na uvamizi wa ardhi ni sugu katika jiji la Dar es Salaam amewataka wananchi wabadilike kujiepusha kujiingiza katika migogoro isiyo ya lazima.
Wakazi wa Kigilagila walilalamika hivi karibuni kuwa awali walitarifiwa fidia zao kuanza kulipwa kutoka Mei mwaka huu lakini mpaka sasa hajaelezwa sababu ya kutolipwa.
Walidai kuwa kutoka wathaminiwe nyumba zao mwaka 1997 pamoja na Kipawa hatujaziendeleza nyingine zimebomoka huku wakisubiri kulipwa fidia bila mafanikio.
Mwanasheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege,Bw. Ramadhani Maleta alipohojiwa wiki iliyopita alitoajibu kama hilo kuwa watalipwa siku chache zijazo baada ya kukamilika kazi ya kupima viwanja na kuchonga barabara za mitaa.

No comments:

Post a Comment