TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 8 October 2010

Msafara wa Mbatia wagongwa tena

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-
Mageuzi, Bw. James Mbatia amepatwa na mkasa mwingine baada ya dereva wake aliyekuwa katika msafara wa kampeni wakienda Mpigi, Kata ya Mbweni kujeruhiwa katika ajali inayodaiwa kuhusishwa kisiasa. Katika ajali hiyo dereva, Rajabu Fikirini alikatwa na vioo shingoni kulikosababisha damu nyingi kuvuja na kupelekwa hospitali kwa matibabu.
Ajali hiyo ni ya pili baada ya ile ya kwanza ambako Jumamosi iliyopita gari analolitumia kupungia wapiga kura kupigwa jiwe ambako mtu mwingine Bw. Alawi (38)kuumizwa kichwani na kuzimia kwa dakika nne.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga hakithibitisha wala kukanusha kutokea matukio hayo na hatua atakayotumia kumpa ulinzi mgombea huyo.

No comments:

Post a Comment