TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday 22 October 2015

Wahitimu Kidato cha Nne wafundwa

Na Peter Mwenda

WANAFUNZI wanaohitimu Kidato cha Nne na kusubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano na vyuo wametakiwa kutumia muda huo kuchagua mienendo mizuri ili wasiangukie kwenye mitego ya ngono zembe,dawa za kulevya na maovu mengine katika jamii.

Mwakilishi wa wazazi wa wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Dkt. Didas Masaburi juzi Dar es Salaam, Bw. Gwamaka Edward alisema jamii imeharibika na vijana wamekuwa wakipuuza tamaduni zao na kushawishika na na tamaduni za watu wa magharibi ambazo hazilengi kuleta maadili ya kitanzania.

Alisema wahitimu wa kidato cha nne ni mwanzo mpya katika safari ya kutafuta taaluma ikikumbukwa kuwa cheti cha kidato cha nne pekee hakikidhi katika dunia ya sasa yenye ushindani katika kupat madaktari, wahandisi, walimu na wanasiasa.

Katika hotuba ya mgeni rasmi, Otieno Igogo aliyewakilishwa na Dkt. Richard Matiko alisema kutokana na ongezeko la watu, Serikali pekee haiwezi kukidhi mahitaji ya elimu nchini hivyo ilifungua milango kwa mashirika na watu binafsi kuanzisha shule ambazo kwa sasa zinatoa elimu nzuri na bora.

Wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne katika hotuba yao nao walisema katika kipindi cha miaka minne ya masomo yao walikumbana na changamoto ya maji na kukosa vitabu vya kujisomea.

Mkuu wa Shule hiyo, Michael Owiti alisema shule hiyo imejipanga kumaliza kero katika shule hiyo kwa kuchimba visima virefu vya maji na kununua vitabu vya kutosha vya kujisomea.

mwisho

No comments:

Post a Comment