TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, October 5, 2015

CAPELABY JOGGING WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA
Wanachama wa kikundi cha Capelaby Jogging wakiwa na watoto wa kituo cha watoto yatima cha Valentine Chiden Home kilichopo njia panda ya buza kitunda Dar es salaam

Mlezi wa kikundi cha Capelaby jogging Latifa Masasi kushoto akitoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Valentine Children Home kilichopo buza njia panda ya kitunda Dar es salaam kulia ni Ester Damian pamoja na Nuru Edward

Mlezi wa kikundi cha Capelaby jogging Latifa Masasi kushoto akitoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Valentine Children Home kilichopo buza njia panda ya kitunda Dar es salaam kwa mlezi wa kituo hicho Sister Janeth Cuthert jana
Mlezi wa kikundi cha Capelaby jogging Latifa Masasi kushoto akitoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Valentine Children Home kilichopo buza njia panda ya kitunda Dar es salaam kwa mlezi wa kituo hicho Lucy Lipenga Jana
Wanachama wa kikundi cha Capelaby Jogging wakiwa na watoto wa kituo cha watoto yatima cha Valentine Chiden Home kilichopo njia panda ya buza kitunda Dar es salaam

BONDIA LULU KAYAGE AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WA DESEMBA 25

Bondia Lulu Kayage kushoto akielekezwa jinsi ya kutupa makonde na kocha Hamisi Belege wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ngumi Ilala

Bondia Lulu Kayage kushoto akielekezwa jinsi ya kutupa makonde na kocha Hamisi Belege wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ngumi Ilala

Tuesday, September 22, 2015

Isere Sports yapata tuzo ya UMITASHUMTA

Na Mwandishi Wetu

WADAU wa Michezo mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kuisaidia Serikali kukuza michezo na kufufua vipaji vya wachezaji katika fani mbalimbali katika shule za msingi na Sekondari.

Akizungumza katika sherehe ya kuwapongeza wachezaji na wadau mbalimbali walioshiriki michezo ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Dar es Salaam juzi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi aliwataka wadau wa michezo kusaidia Serikali kufufua vipaji vya wachezaji.

Katika sherehe hizo ambazo mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam waliotwaa ubingwa wa jumla za mashindano hayo yaliyofanyika mkoa wa Mwanza mwaka huu,Meneja wa timu ya UMITASHUMTA ya Mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Ally alisema mikoa mingi ilidhamiria kupata ushindi huo lakii wao walijiandaa zaidi.

Mmoja wa wadau waliopata tuzo hiyo Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally ambao ni wauzaji wa vifaa michezo nchini aliahidi kuongeza vifaa vyenye ubora kwa bei nafuu ili mwakani mkoa huo uendelee kuwa mabingwa.

Mkoa wa Dar es Salaam uliochukua ushindi wa jumla kwa kutwaa medali  26 katika michezo mbalimbali lakini ikiwemo soka ya wanawake lakini ilijikuta inafungwa katika mchezo wa soka ya wamaume baada ya kupachikwa bao 1-0 na wenyeji Mwanza.

mwisho


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi (kushoto) akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally (kulia) kwa ushiriki wao uliofanikisha ushindi wa jumla wa UMITASHUMTA kwa mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni katika mashindano yaliyofanyika Mwanza.Sherehe hizo zilifanyika juzi jijini Dar es Salaam (Picha na Peter Mwenda)

Monday, September 21, 2015

Wasanii wachangamkia misingi ya nyumba SHIWATA

Na Peter Mwenda, Mkuranga
 

WASANII na wanamichezo wameupongeza Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kubuni njia ya kuwakomboa wasanii kumiliki ardhi kwa kuwamilikisha viwanja bure katika kijiji cha Wasanii Mkuranga baada ya kulipia msingi wa nyumba kwa sh. 200,000.
 

Baadhi ya Wasanii waliomilikishwa misingi hiyo juzi waliambia Majira kuwa mpango huo mpya ni mzuri na mkombozi kwao kwa vile kipato chao si cha uhakika kulinganisha na mpango uliokuwa umebuniwa awali wa msanii kuchangia mpaka akamilishe kulipia nyumba ndipo amilikishwe.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema hiyo ni ofa kwa mwanachama ambaye atapata nusu hekari kama atakuwa amelipa sh. 200,000 za kujengewa msingi wa nyumba ya chuma kimoja kutumia matofali ya saruji."Hii ni ofa maalum kwa wanachama wetu kupata kiwanja bure kama atakuwa amelipia benki sh. 200,000 za kumjengea msingi wa nyumba yake katika kijiji chetu Mwanzega Mkuranga ambako mpaka sasa kati ya hekari 300 tulizonazo za makazi ni hekari kumi tu zimejengwa nyumba 120,." alisema Taalib.
 

Alisema katika misingi hiyo wanaotaka kumaliza nyumba zao gharama yake jumla itakuwa sh. 850,000 kwa nyumba ya chumba kimoja, sh. 3,800.000 kwa nyumba ya vyumba viwili na sh. 6,400,000 kwa nyumba vya vyumba vitatu na sebule.


Mwenyekiti Taalib alisema bado nafasi iko wazi kwa wasanii wanaotaka kuwekeza kwa kujenga shule, hospitali, kumbi za starehe na viwanja vya nmichezo wanakaribishwa.


Alisema makundi ya wasanii ambao bado hawajajiunga na mtandao huo watapewa ofa ya kulipa sh. 70,000 kwa mtu mmoja katika vikundi na msanii mmoja mmoja atajiunga kwa sh. 120,000 ambapo atapewa pia katiba ya mtandao huo.

mwisho

Mwenyekiti wa SHIWATA Cassim Talib (kulia),akiwa amebeba tofali na wasanii wengine kwa ajili ya kujenga misingi ya nyumba kwa gharama ya sh.200,000 ambapo atapewa kiwanja cha miguu 35 kwa 35 bure katika kijiji cha Wasanii Mwanzega Mkuranga mkoa wa Pwani ambako Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unamiliki hekari 300 za makazi.(Picha na Peter Mwenda).
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib (kulia) akifafanua kwa wasanii namna atakavyomilikishwa eneo baada ya kulipia msingi wa chumba kimoja kwa gharama ya sh. 200,000 kwa kupewa kiwanja cha ukubwa wa miguu 35 kwa 35 bure kwa ajili ya kujenga nyumba kubwa katika Kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga mkoa wa Pwani ambako Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unamiliki hekari 300 za kujenga nyumba za makazi.Picha na Peter Mwenda.