TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday 22 October 2015

Kawe Jogging yaipa tuzo Isere Sports

Na Peter Mwenda

KLABU ya Mbio za polepole (jogging) ya Kawe jijini imeizawadia tuzo ya heshima Kampuni ya Isere Sports kwa mchango wake uliofanikisha kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro Marathon mwaka huu.

Katibu wa Kawe Jogging, Alhaj Seif Muhere akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka minne ya klabu hiyo juzi Dar es Salaam alisema Kampuni ya Isere Sports imepata heshima hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo mapema mwaka huu.

Katika sherehe hizo ambazo zilisindikizwa na Kikundi cha Wakali Music Taarab zilizofanyika ukumbi wa Nikkata Resort, Mbezi Juu, klabu 15 za Jogging kutoka maeneo mbalimbali y jiji la Dar es Salaam zilihudhuria.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally alisema amefurahi kupata tuzo hiyo na kuahidi kusadia klabu ya Kawe Jogging kwani inaokoa maisha ya jamii inayoshiruki mazoezi hayo kujikinga na maradhi.

"Michezo ya jogging inaokoa watu wengi kujiepusha na maradhi ya Kisukari, Shindikizo la damu (BP) na magonjwa mengine" alisema Isere.

Alisema ili Kawe Jogging ifanye vizuri katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon mwaka huu anaomba kampuni nyingine na taasisi za umma kushirikiana naye kufadhili klabu hiyo.

Klabu ya Kawe Jogging ndiyo pekee kutoka nchi za Afrika Mashariki kushiriki inayoshiriki mbio za Kilimanjaro Marathon za km 5 kwa mwaka wa tatu mfululizo inaomba wahisani wengine kujitokeza kuisaidia kwa hali na mali.


mwisho.


No comments:

Post a Comment