TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 9 October 2015

PPF kuwakatia wasanii Bima ya Afya

Na Peter Mwenda
WASANII wa fani mbalimbali nchini leo watapata fursa ya kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Pensheni (PPF) kwa kupata dhamana ya huduma za Bima ya Afya na Mikopo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa katika mkutano huo wa wanamichezo wote unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Hosteli ya Vijana, Kinondoni umelenga kuwasaidia wasanii kimaisha.

Taalib alisema mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi kwa Upande wa SHIWATA pia utakuwa wenye manufaa kwa wasanii watakaohudhuria kwa maendeleo yao ya baadaye ambao watapewa ofa maalum.

Alisema ofa ya SHIWATA ni kwa wanachama watakaojiunga kwa mara ya kwanza watalipa sh. 20,000 badala ya sh. 115,000 na kupewa kiwanja bure chenye ukumba wa miguu 35 kwa 35 kwa ajili ya kujenga nyumba ya makazi katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ambako mpaka sasa hekari 290 katika ya 300 hazipata wawekezaji.

Alisema PPF nao katika mkutano huo watawatoa elimu ya jinsi wasanii watakavyojiunga na Bima ya Afya huduma ya matibabu ambayo itaanza kutolewa baada ya msanii kulipia sh. 60,000 kwa awamu tatu.

Taalib alisema PPF pia watatoa mikopo mbalimbali ili kuwakwamua wasanii kimaisha ambako mpaka sasa SHIWATA inayo wanachama wasanii 8,000 kati yao wamejenga nyumba 120 katika kijiji cha Mwanzega, na wengine wanamiliki mashamba katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga.

Mwenyekiti Taalib alisema katika mkutano huo wasanii watatakiwa kuvaa mavazi rasmi ya wasanii na siyo sare za vyama vya siasa.


mwisho

No comments:

Post a Comment