TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday 7 October 2015

SHIWATA,PPF yawaandaa wasanii kupata Bima ya Afya

Na Peter Mwenda

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Pensheni (PPF) wameandaa mkutano wa wasanii na wanamichezo wote Jumamosi Oktoba 10 kwenye ukumbi wa Hosteli ya Vijana, Kinondoni wenye lengo la kuwasaidia kimaisha.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa katika mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa wenye manufaa kwa wasanii watakaohudhuria kwa maendeleo yao ya baadaye pia kutakuwa na ofa maalumu kutoka SHIWATA.

Alisema ofa itakayotolewa na SHIWATA ni kwa wanachama watakaojiunga kwa mara ya kwanza watalipa sh. 20,000 badala ya sh. 115,000 na kupewa kiwanja bure cyenye ukumbwa wa miguu 35 kwa 35 kwa ajili ya kujenga nyumba ya makazi katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ambako mpaka sasa hekari 290 katika ya 300 hazipata wawekezaji

Alisema PPF nao katika mkutano huo watawatoa elimu ya jinsi wasanii watakavyojiunga na Bima ya Afya huduma ya matibabu  ambayo itaanza kutolewa baada ya msanii kulipia sh. 60,000.

Taalib alisema PPF pia watatoa mikopo mbalimbali ili kuwakwamua wasanii kimaisha ambako mpaka sasa SHIWATA inayo wanachama wasanii 8,000 kati yao wamejenga nyumba 120 katika kijiji cha Mwanzega, na wengine wanbamiliki mashamba katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga.

Mwenyekiti Taalib alisema katika mkutano huo wasanii watatakiwa kuvaa mavazi rasmi ya wasanii na siyo sare za vyama vya siasa.

mwisho

No comments:

Post a Comment