TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday 21 September 2015

Wasanii wachangamkia misingi ya nyumba SHIWATA

Na Peter Mwenda, Mkuranga
 

WASANII na wanamichezo wameupongeza Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kubuni njia ya kuwakomboa wasanii kumiliki ardhi kwa kuwamilikisha viwanja bure katika kijiji cha Wasanii Mkuranga baada ya kulipia msingi wa nyumba kwa sh. 200,000.
 

Baadhi ya Wasanii waliomilikishwa misingi hiyo juzi waliambia Majira kuwa mpango huo mpya ni mzuri na mkombozi kwao kwa vile kipato chao si cha uhakika kulinganisha na mpango uliokuwa umebuniwa awali wa msanii kuchangia mpaka akamilishe kulipia nyumba ndipo amilikishwe.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema hiyo ni ofa kwa mwanachama ambaye atapata nusu hekari kama atakuwa amelipa sh. 200,000 za kujengewa msingi wa nyumba ya chuma kimoja kutumia matofali ya saruji.



"Hii ni ofa maalum kwa wanachama wetu kupata kiwanja bure kama atakuwa amelipia benki sh. 200,000 za kumjengea msingi wa nyumba yake katika kijiji chetu Mwanzega Mkuranga ambako mpaka sasa kati ya hekari 300 tulizonazo za makazi ni hekari kumi tu zimejengwa nyumba 120,." alisema Taalib.
 

Alisema katika misingi hiyo wanaotaka kumaliza nyumba zao gharama yake jumla itakuwa sh. 850,000 kwa nyumba ya chumba kimoja, sh. 3,800.000 kwa nyumba ya vyumba viwili na sh. 6,400,000 kwa nyumba vya vyumba vitatu na sebule.


Mwenyekiti Taalib alisema bado nafasi iko wazi kwa wasanii wanaotaka kuwekeza kwa kujenga shule, hospitali, kumbi za starehe na viwanja vya nmichezo wanakaribishwa.


Alisema makundi ya wasanii ambao bado hawajajiunga na mtandao huo watapewa ofa ya kulipa sh. 70,000 kwa mtu mmoja katika vikundi na msanii mmoja mmoja atajiunga kwa sh. 120,000 ambapo atapewa pia katiba ya mtandao huo.

mwisho

No comments:

Post a Comment