TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 3 July 2015

Ezekiel Malongo hatunaye tena duniani

Na Mwandishi Wetu

MTANGAZAJI mahiri na machachari wa michezo aliyewahi kutamba katika medani ya habari za michezo nchini, Ezekiel Malongo amefariki dunia katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kuugua kwa muda.

Malongo ambaye anafahamika sana kwa waandishi na watangazaji wenzake kwa manjonjo ya kutangaza katika kipindi cha michezo cha Redio Tanzania alivyokuwa na ujasiri wa kuwahoji viongozi wa FAT wakati huo.

 Katika kipindi hicho Katibu Mkuu wa FAT alikuwa Michael Wambura, Katibu Mkuu wa Kamati ya muda ya FAT, Mwina Kaduguda, Katibu Mkuu, Ismail Adena Rage na Mwenyekiti Muhidin Ndolanga.

 Malongo aliwika sana hata katika bendi maarufu ya Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae na nyingine nyingi ambazo alifanya nazo kazi.

Mimi kwa upande wangu alikuwa rafiki yangu wa karibu na tulifanya naye kazi kwa pamoja.

mwisho



No comments:

Post a Comment