TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday 13 July 2015

Magufuli mgombea urais CCM 2015

Magufuli afufua matumaini ya watanzania

.Ndiye mgombea Urais kupitia CCM 2015

.Awabwaga wenzake 38


Na Mwandishi Wetu


WAZIRI wa Ujenzi, John Pombe Magufuli amechaguliwa na chama chake kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Magufuli ambaye aliingia tano bora akiwa na Januari Makamba, Benard Membe, Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ally aliingia kwenye tatu bora akiwa mwanaume pekee.

Magufuli aliingia tatu bora akiwa na Migiro na Balozi Amina Salum Ally ndipo alipozoa kura 2,104 ambazo ni sawa na asilimia 87.4 na kuwapita kwa kura nyingi Amina aliyepata kura 253 na Migiro kura 59.

Katika hotuba yake Magufuli ambaye aliitwa jina la utani na Rais Jakaya Kikwete kuwa tingatinga aliwaahidi watanzania kuwa kazi waliyomtuma ameipokea na ataifanya kwa uaminifu mkubwa.


mwisho

No comments:

Post a Comment