TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday 23 February 2015

Isere Sports kuagiza vifaa Riadha nchini

Na Mwandishi Wetu,Morogoro


MAOFISA michezo na Maofisa Elimu wa mikoa ya Tanzania wameombwa kushirikiana na wenyeviti wa mchezo wa riadha katika kufufua mchezo huo kutoka ngazi ya shule za msingi, Sekondari na vyuoni.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui       aliyasema hayo katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa tathmini wa mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari (UMISETA) yanayosimamiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini hapa.

Alisema imefika wakati kwa wadau wenye kupenda nchi yao imereshe heshima ya zamani achangie kufufua mchezo huo kwa kuwashauri vijana wenye vipaji vya riadha kuanza mazoezi.

Nyambui alisema riadha ambayo ilitangaza Tanzania katika mashindano ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki na marathon unazidi kupoteza umaarufu kwa sababu hakuna mikakati madhubuti ya kufuatilia wanamichezo wenye vipaji kutoka ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Alisema anafarijika kuona kuwa baada ya miaka mingi kupita Tanzania mwaka jana katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Scotland mtanzania Basil John aliingia fainali ya mita 1500 kwa kushika nafasi ya nane kati ya 12 walioingia fainali.

Alisema mchezaji huyo ni wa kwanza kufika hatua hiyo baada ya miaka 40 kutoka Filbert Bay avunje rekodi ya mita 1,500 duniani.

Katibu Nyambui alisema mchezo wa riadha hauna wafadhili kama ilivyo michezo ya soka lakini amejitahidi kushawishi kampuni ya Isere Sports isaidie kuwauzia wachezaji wa riadha vifaa kwa bei ya chini.

"Tumekubaliana na Kampuni ya Isere Sports iagize na kuwauzia wanariadha vifaa vya michezo kwa bei ya kawaida ili wamudu kununua viatu na jezi za " alisema Nyambui.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ni kweli wameingia makubaliano na Shirikisho la Riadha kuagiza vifaa vya mchezo huo na kuwauzia kwa bei ya chini ili kufufua mchezo huo.


mwisho.


No comments:

Post a Comment