TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 11 February 2015

Mtoto aomba msaada wa tiba,chakula

Na Peter Mwenda

MTOTO Winifrida Michael (13) mkazi wa Keko Mwanga, Dar es Salaam anaomba wasamaria na wengine wenye mapenzi mema kumsaidia kupata fedha za matibabu na kujikimu baada ya kupata ugonjwa wa ajabu uliosababisha kuvimba mguu wa kulia.

Mama wa mtoto huyo, Agatha Mndolwa aliambia majira kuwa mwanae huyo amekuwa halali akilalamika maumivu na amewahi kulazwa katika hospitali ya Amana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Agatha alisema uvimbe katika mkuu wa mwanae ulijitokeza Januari mwaka hana baada ya kujigonga kwenye ukingo wa kitanda na ukaanza kuvimba kidogo kidogo akiwa kijijini kwao Maramba mkoani Tanga.

Alisema alipelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga ya Maramba ambako alilazwa na kufanyiwa uchunguzi ambao haikuonekana kinachomsumbua.

Mama huyo alisema alimleta mwanae Dar es Salaam na kumpeleka hospitali ya Amana na baadaye Muhimbili ambako alitibiwa lakini bado hali yake haijarudi kuwa ya kawaida.

Alisema huduma ya kumsaidia mwanae imekuwa ya shida sana baada ya kusimamisha kazi ya mama lishe iliyokuwa inamsaidia.

Agatha alisema aliwahi kujitokeza msamaria mwema aliyejitolea kumpatia mashine ya Serojem ambayo ilimsaidia kupunguza maumivu ambayo nayo iliharibika baada ya ukuta wa nyumba waliyokuwa wakiishi kuanguka.

Alisema mwenye nia ya kumsaidia wawasiliane naye kupitia simu 0719 654143 au 0655 990013 Bakari Mrosa ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Keko Mwanga B.

mwisho

No comments:

Post a Comment