TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Sunday, 27 January 2013

Wanahisa NICOL wamtaka Felix Mosha aachie ngazi

 Na Mwandishi Wetu

WANAHISA wa Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa NICOL wamemfukuza aliyekuwa Mwenyekiti Bw.Felix Mosha pamoja na uongozi wake na kumtaka akabidhi mali zote kwa uongozi mpya kabla ya Aprili 9 Mwaka huu vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
 

Wakizungumza katika kikao kilichoandaliwa Dar es Salaam jana na uongozi mpya wa NICOL pamoja na Wanahisa wamesema mbali na kukabidhi mali zao pia wamemtaka akabidhi ofisi na vitendea kazi yakiwemo makabrasha ili waendelee kufanya kazi.


Katika kikao hicho Wanahisa hao wamewaagiza Jaji Mark Boman, Mzee Anord Kileo,Balozi Paul Rupia,Bw.Reginard Mengi na Balozi Nyaki kumwambia Bw.Mosha aondoke kwa hiyari kinyume cha hapo watampeleka polisi na mahakamani.

Pia wameuagiza uongozi mpya kutoa taarifa kwa Kampuni zinazofanya kazi na NICOL kwa sasa kuwa Bw.Mosha si Mwenyekiti tena wa Kampuni hiyo.

Sambamba na hilo Wanahisa hao wameuagiza uongozi mpya kufanya thimini ya kesi zilikuwa mahakamni na kuhakikisha zile zote ambazo hazina tija kwa NICOL zifutwe.

Hata hivyo wametoa onyo kwa Bw.Moshi kuacha mara moja kuingilia kati mambo ya Kampuni hiyo.

Naye Mwenyekiti wa NICOL Bw.Gideon Kaunda alisikitishwa na kitendo cha Bw.Mosha kukataa kutoka katika ofisi hiyo na kusababisha kufanya kazi bila ya kuwa na ofisi wala vitendea kazi.

Alisema kitendo hicho ni kuwadhurumu wahahisa haki zao kwani wao ndio wenye kampuni hiyo na sio ya mtu binafsi.

Pia alisikitishwa na kitendo cha Bw.Mosha kuwazuia wanahisa kutoudhuria kikao hicho kwa madai kuwa ni batili.

Awali alisema chanzo cha matatizo yanayojitokeza hivi sasa ni kutokana na uozo wa kiutendaji pamoja na kutoheshimu maamuzi ya Wanahisa.

Kwa upande wa Meneja wa Mpito wa NICOL Bw.Kinoni Wamunza alisema mpaka kampuni hiyo imepata hasara ya zaidi ya Bil.9.8 ndani ya miaka mitatu mwaka 2007 walipata hasara ya bil.1.9 mwaka 2008 bil.4.5 na mwaka 2009 bil.3.4.

Alisema hasara hiyo imesababishwa na kuchelewa kwa mahesabu hiyo ni kutokana na kutokuwa na ushirikiano ndani ya kampuni.
 

Wakati huohuo mmoja wa mwanzilishi wa Kampuni hiyo Jaji Boman alisikitishwa kuona NICOL ipo katika hali mbaya ya kuwa na madeni pamoja na kutokuelewana kwa viongozi.

"Hivi wanahisa wetu walioingia ndani ya miaka 10 tutawaambia nini ukizingatia tuliwafuata watu wa kawaida tu na sio matajiri tena walikubali kuuza hadi kuku na bata zao wakiwemo mbuzi zao"alisema  Jaji Boman.

Hivyo alimuomba Bw.Mosha aondoke madarakani kwani haiwezekani kukaa miaka kumi peke yake katika kampuni ya umma.

"Nivema akaondoka ili tuanze upya kwa lengo la kujipanga tuone vipi itaendelea kusonga mbele."alisema Bw.Boman.

    

No comments:

Post a Comment