Walemavu wapewe ruzuku kama vyama vya Siasa
Na Peter Mwenda
SERIKALI imetakiwa kuweka sheria ya kutoa ruzuku kwa watu wenye ulemavu ili kuwarahisishia kuendesha miradi yao na kujenga vyama vyao.
Hayo yalisemwa na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika warsha ya wiki moja ya kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi ya utunzaji wa fedha uliofanyika Dar es Salaam.
"Kama vyama vya siasa wanapata ruzuku kwa nini walemavu tusipate fedha kwa ajili ya kuturahisishia kuendesha vyama mfano sisi albino zitusaidie kununulia losheni,kununua kofia,miwani ya jua na nguo" alisema Bw. Mussa Faraji ambaye ni Mweka Hazina wa Chama cha Albino Mkoa wa Dar es Salaam (TAS).
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gabriel Aruga alisema jamii inatakiwa kupata elimu kuwa walemavu wanaweza kufanya kazi kama watu wengine.
Alisema albino nao wajue kuwa wao ni watu kama wengine ambao wanaweza wa kufanya kazi sawa na watu wasiokuwa walemavu.
Alisema kutokana na uleamavu wao wanatakiwa kupewa upendeleo katika kupata elimu kwa kuchapishiwa vitabu vyenye maandishi makubwa na wanafunzi kuwekwa viti vya mbele darasani kutokana na uono hafifu.
Bw.Aruga alisema pamoja na jitihada hizo bado kuna unyapaa katika ajira kwa albino kwa sababu bado jamii inaona kuwa hawana uwezo wa kufanya kazi tofauti la ukweli kwamba wao ni watu wenye uwezo mkubwa.
Pia wameiomba Serikali kutenga maeneo maalum maalum kwa ajili ya walemavu ili wawe na mfuko ambao utawasaidia kupata kipato kwa urahisi.
mwisho
No comments:
Post a Comment