TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 5 October 2012

TUESDAY KUINGIA KATIKA USAMBAZAJI WA FILAMU.


Jumba la Dhahabu
Filamu ya kwanza kusambazwa na jumba la Dhahabu.
MKURUGENZI wa kampuni ya Tuesday Entertainment Ltd, Tuesday kihangala ‘Mr. Chuzi’ ameieleza FC kuwa kampuni yake kwa sasa imezidi kujitanua zaidi baada ya kufungua kampuni nyingine inayojishugulisha na usambazaji wa filamu na tamthilia na kwa kuanza kampuni hiyo imeanza na tamthilia iliyotamba sana ya Jumba la Dhahabu.
Philipo Michael
Kojack mmoja wa waigizaji wa tamthilia hiyo ya jumba la Dhahabu.
Ahmed Ulotu
Mzee Chilo naye ndani
Jumba la Dhahabu
Jumba la Dhahabu sokoni
“Katika kulinda maslahi na muda pia kwa sasa kampuni imeongeza kitengo kingine kwa ajili ya kusambaza kazi zetu, na hivi ninavyoongea na wewe tayari kampuni inasambaza kazi yetu ya Jumba la Dhahabu na inafanbya vizuri sana katika soko la filamu,”anasema Mr. Chuzi. Kampuni ya Tuesday Entertainment ndio kampuni inayoongoza kwa sasa kumiliki wasanii wengi wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu, kampuni hiyo kwa sasa ipo katika maandalizi makali ya urekodiji wa tamthilia ya Jumba la Dhahabu sehemu ya pili na inatarajia kuanza kuruka hivi karibuni kwa kupitia katika kituo cha Televisheni ya Taifa TBC 1.
Jumba la Dhahabu itakuwa ikiruka kwa siku tano mfululizo kuanzi Jumatatu hadi Ijumaa kwa wiki nzima, jambo ambalo litasaidia tamthilia za nyumbani kushindana na zile za nje ambazo upewa muda mkubwa katika Televisheni zetu za hapa nyumbani.

No comments:

Post a Comment