TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 5 October 2012

HAYA NI MAISHA YANGU- MAMA DIDII.


Dometria Alphonce
Mtayarishaji na mwigizaji wa filamu Swahiliwood Dometria 'Mama DD'
MJASIRIAMALI na mwigizaji wa filamu Swahiliwood Dometria D. Alphonce ‘Didii’ ameieleza FC kuwa filamu ya Kua uyaone ni maisha yake aliyopita katika Ndoa yake na kuamua kuandika hadithi inayohusu maisha yake jambo ambalo anaamini kuwa filamu ya Kua Uyaone itakuwa faraja kwa wale wote walikubwa na matatizo ya ndoa.
Bi. Mwenda, Parcho Mwamba, Dometria Alphonce
Bi. Mwenda, Parcho Mwamba, Dometria Alphonce wakiwa katika picha ya pamoja
Dometria Alphonce
Dometria Alphonce akiwa katika pozi.
“Siku zote katika sanaa ya filamu nimekuwa nikishiriki filamu za watayarishaji wengine lakini kwa sasa nimeamua kuandaa filamu yangu mwenyewe na inahusu maisha yangu halisi, huu ni mwanzo kwangu kuingia rasmi katika tasnia ya filamu nikiwa kama muandaaji na mwigizaji pia,”anasema Didii. Filamu ya Kua Uyaone imetayarishwa na kampuni ya DD Entertainment na kutengenezwa na JAS Media chini ya mtaalam Gia, katika filamu hiyo wasanii walioshiriki ni Seif Mbembe, Mzee Korongo, Bi. Kidide, Pancho Mwamba, Didi mwenyewe na wasanii wengine kibao, muongozaji wa filamu hiyo ni mkali wa filamu za mapigano Moses Mwanyilu.

No comments:

Post a Comment