TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 5 October 2012

MABINGWA WA SAFARI POOL 2012 KAYUMBA KLABU YAPOKELEWA KWA SHANGWE DAR.


Mabingwa wa Safari Pool Taifa 2012, Kayumba Klabuwakishangilia na Kikombe kwenye gari la wazi mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam

Mabingwa wa Safari Pool Taifa 2012, Kayumba Klabu  na baadhi ya mashabiki wa Pool Wilaya ya Igunga wakishangilia na Kikombe walipokuwa wakirejea jijini Dar es Salaam mara baada ya kutwaa ubingwa huo jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Mabingwa wa Safari Pool Taifa 2012, Kayumba Klabu wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam

 Mabingwa wa Safari Pool 2012, Kayumba Klabu wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi,Meneja wa Bia ya Safari Lager na baadhi ya viongozi wakati wa hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa, Henry Lihaya akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza Mabingwa Klabu ya Kayumba iliyofanyika Nyantare Tabata jijini Dar es Salaam.

KATIBU Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa, Henry Lihaya amewataka Chama cha Pool Taifa(TAPA),Wachezaji na wapenzi wa mchezo kutunza na kuheshimu uafadhili wa Bia ya Safari Lager katika mchezo wa Pool.
Lihaya aliyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza mabingwa wa mchezo huo 2012 Kayumba kutoka Mkoa wa kimichezo wa Ilala yenye makazi yake Buguruni jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Safari Lager iliyofanyika katika Klabu ya Nyantare Tabata.
Alisema Lihaya ondoeni migogoro isiyokuwa na maana ndani ya chama na mmuendeleze chama inavyopaswa,Tanzania tunayo michezo mingi sana lakini hamuoni ni upendeleo kiasi gani Safari Lager anapoteza mamiliono ya pesa kudhamini mchezo wa pool,jengeni chama tunzeni udhamini na Tangazeni Safari Lager popote mlipo ili kurudisha kwa Safari Lager pale anapotoa.
Lihaya alimaliza kwa kuseme ni wakati sasa wa kuutoa mchezo wa pool katika mazingira ya Bar ili kutoa taswira ya watu kuita mchezo wa walevi na mwaka kesho mchezo huo uchezwe mikoa yote ya Tanzania na si mikoa 16 tu,na pia mchezo wa pool sasa uingizwe mashuleni.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Katibu wa chama cha Pool, Amos Kafwinga alishukuru TBL kwa uzamini wa mashindano Safari Pool Taifa 2012 mpaka kufiaki tamati na pia kumuomba mzamini asichoke kuwasaidia hasa kwenye mashindano ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika Wingereza ambapo timu ya Taifa inatarajia kushiriki.
Kayumba walipokelewa kwa maandamano yaliyoanzia Ubungo mpaka Klabuni kwao Kayumba yenye makazi yake Buguruni kwa Mnyamani na baadae kwenye Tafrija fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Safari Lager.

No comments:

Post a Comment