TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 3 October 2012

REA YASAMBAZA UMEME NEWALA
Na Peter Mwenda, Newala
WAKALA wa Usambazaji wa Nishati Vijijini (REA) wilayani hapa unatarajia kuwasambazia umeme kwa wateja 2,000 hadi  kufikia Desemba mwaka huu.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)wilayani hapa Bw. Basilius Kayombo aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mradi wa REA ambao umeanza kutekelezwa katika vijiji vitano wananchi wanatakiwa kuchukua fomu za kujiandikisha na kulipia sh. 99,000 ambazo ni gharama ya kuingiza umeme.
 Bw.Kayombo alisema wananchi watakaonufaika na mradi huo ni wale ambao nyumba zao hazizidi mita 30 kutoka njia kuu ya umeme na taasisi za umma na kidini zitapewa kipaumbele.
 Alisema mradi katika kila kijiji mradi huo utatumia sh. Mil. 54.9 na kuvitaja vitakavyonuika ni Makonga, Lengo,Mtangalanga,Likuna na Mikangaula ambao wataanza kuunpata umeme kuanza Oktoba 5 mwaka huu.
 Baadhi ya wananchi wakitaka kujua ufafanuzi wa uingizaji umeme kwenye nyumba za nyasi, Kaimu Meneja wa TANESCO mkoa wa Mtwara, Bw. Bw. Daniel Kyando alisema nyumba zilizoezekwa kwa nyasi haziingiziwa umeme.
 Alisema wateja ambao nyumba zao zimejengwa na kuezekwa nyasi wazijenge upya na kuezeka bati ili wanufaike na mradi huo.
 Bi. Asha Nalamba alisema nyumba yake ya nyasi ataibadilisha na kuezeka bati ili aingize umeme ambao alisema ni mafanikio makubwa katika jamii ya wakazi wa mkoa wa Mtwara.

No comments:

Post a Comment