BWENI LA WASICHANA LATEKETEA KWA MOTO TANDAHIMBA
Na Peter Mwenda, Tandahimba
WANAFUNZI 80 wa kike hawana mahali pa kuishi baada ya bweni lao kuuungua moto na kuteketeza vitu vyao vyote vilivyokuwemo baada ya moto mkubwa kuzuka.
Katika tukio hilo lililozusha kizaazaa na kusababisha wanafunzi kuingiwa kiwewe kukimbia hovyo wakiwa wanaokoa mali zao moto huo ulizuka saa 3 asubuhi katika Chuo cha Kilimo na Mifugo Naliendele.
Gari la kuzima moto SU 37036 la Mamlaka ya Bandari Mtwara lilifika wakati bweni hilo lililokuwa na vitu mbalimbali vya wanafunzi hao vikiwa vimeteketea kabisa lakini hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Mwanafunzi Hemed Abdallah aliyeshuhudia tukio hilo alisema ulianza kuonekana moshi mkubwa katika bweni hilo ambako ghafla wanafunzi wa kike wanaoishi humo walianza kujiokoa lakini hawakufanikiwa kuokoa mali zao.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Bw. Alfred Oseah aliyefika eneo la tukio alisema chanzo cha moto bado hakijajulikana lakini taarifa za awali kutoka kwa wanafunzi wa chuo hicho walidai ni hitilafu ya umeme.
Mkuu wa Chuo cha Nalindele Bw.Waziri Ali alisema moto huo ulitokea ghafla na kushindwa kuuzima baada ya kuwazidi nguvu hali wao wakiwa hawana vifaa vya kuzima.
No comments:
Post a Comment