TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 7 November 2011

Prince Charles ataka Dar ipate majiji dada Uingereza

Na Peter Mwenda

MFALME wa Wales na mrithi pekee wa kiti cha Ufalme na mtoto wa Malkia wa Uingereza, Prince Charles amemshauri Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi kujenga ushirikiano na mmoja ya majiji ya Uingereza kushirikiana ili kuleta maendeleo.

Dkt. Masaburi alitoa historia ya Jengo la Karimjee ambalo lilijengwa na serikali ya Uingereza mwaka 1916 wakati ikitawala Tanzania na kuzindua miaka 50 ya uhuru.

Prince Charles alifurahishwa na historia ya Karimjee na kusikia kuwa baba yake aliwahi kutembelea jengo hilo na ndipo Raisa wa Kwanza Hayati Julius Nyerere ndipo alipoapishwa.

Katika ziara hiyo Prince Charles alizindua stempu za mpya Shirika la Posta Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru na kuzawadiwa vitabu vya Sayansi kutoka kwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa.

Prince Charles ambaye atakuwepo nchini kwa ziara ya siku nne akifuatana na mkewe Camila alisema Jiji la Dar es Salaam linatakiwa kuwa uhusiano wa majiji dada nchini Uingereza ili kupata mbinu za kupata maendeleo.

"Prince ametaka tuwe na ushirikiano na majiji nchini Uingereza hiyo tutafanikiwa sana kupata msaada wa kubadilisha jiji kuwa la kisasa zaidi" alisema Dkt. Masaburi.

Awali akiwasili Ikulu jana, Prince Charles alipokelewa na Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma na viongozi wengine wa kitaifa wanafunzi wa shule za sekondari Dar es Salaam na baadaye alikwenda makao makuu ya Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).


Prince Charles ambaye aliwasili juzi na kupokelewa na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe atafanya ziara ya Zanzibar na Arusha.

mwisho

No comments:

Post a Comment