Na Peter Mwenda
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama Tanzania unakabiliwa na uhaba wa damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji kuongezewa damu hospitalini.
Meneja wa Mpango wa Damu Salama Tanzania, Dkt. Efesper Mkya aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa damu inayohitajika kwa matumizi kwa mwaka mmoja ni uniti 350,000-400,000 lakini inayopatikana haizidi uniti 120,000.
Alisema watanzania wengi ambao ni watoto wa chini ya umri wa miaka mitano, wajawazito,wagonjwa wa saratani na majeruhi wa ajali wanahitaji wasamaria wema kujitolea kutoa damu kwa hiari ili kuokoa maisha yao.
Dkt. Nkya alisema kutokana na upungufu huo Mpango wa Admu Salama unashindwa kutoa huduma ipasavyo hivyo kulazimika ndugu wa wagonjwa kuchangia damu pindi ndugu yzao wanapopatwa tatizo.
Alisema hata hivyo Mpango wa Damu Salama unatoa wito kwa watanzania ambao umri wao ni kati ya miaka 18 hadi 65 wanaombwa kujitokeza kujitolea damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.
Dkt. Nkya alisema Mpango wa Damu Salama unawashukuru wanafunzi wa Shule za Sekondari nchini wanaoendelea kujitolea kutoa damu katika vituo vyao saba nchini.
Alisema mikakati ya mwaka huu ni kupata uniti 180,000-200,000 katika kipindi kinachoishia mwaka huu.
Dkt. Nkya alisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umesambaza tangazo katika kila hospitali la kuonya kuwa Damu Haiuzwi na inatolewa bila malipo hivyo kuwatahadharisha wananchi na wagonjwa kutpiga simu kwa wahusika ambao namba zao zipo katika tangazo hilo.
mwisho
No comments:
Post a Comment