TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 1 August 2011

Mpiga picha majira kortini kwa kutanua barabarani

Na Peter Mwenda

MPIGA na mwandishi mkongwe wa gazeti la Majira, Bw. Nyakasagani Masenza amefikishwa katika mahakama ya wilaya Ilala kwa tuhuma za kutanua barabarani na kukaidi amri ya trafiki ya kumtaka arudishe gari lake alikotoka.

Akisomewa mashataka mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Bw. Nyakasagani anadiwa kuwa leo saa 2.30 katika maeneo ya Vingunguti alitanua barabara na trafiki alipomtaka kurudi alikotoka aligoma.

Shuhuda wa tukio hilo mpiga picha wa Jambo Leo, Bw.  Richard Mwaikenda aliyekuwepo katika gari hilo alisema Bw. Nyakasagani baada ya kuamriwa kurudisha gari nyuma alisogea mbele ili alipaki pembeni ili ajieleze lakini ghafla alikuja trariki mwingine na kumkunja shati na kumtoa ndani ya gari.

Haraka haraka aliingizwa kwenye Defender na kukimbizwa kituo Kikuu cha Trafiki, na kufunguliwa jalada la mashtaka na kupelekwa mahakamani kazi iliyofanyika ndanio ya nusu saa.

Katika jitihada za kumwekea dhamana Bw. Mwenda wa gazeti la majira akiwa na barua ya dhamana kutoka Business Times (majira) barua nyingine ambaye alikuwa aje nayo Mwaikenda ilichelewa kufika mahakamani hapo hivyo hakimu kuamuru mshitakiwa aende mahabusu ya Segerea hadi kesho saa mbili asubuhi.

Pamoja ya kuomba Hakimu alegeze masharti hata baada ya barua hiyo kufika alisema hawezi kurudisha mahakamani mara mbili baada ya kufunga jalada hilo, hivyo iliombwa iandikwe hati ya kumrejersha mahakamani "Remove Order" ambayo itamrudisha mtuhumiwa huyo mahakamani kesho. Kesi yake itatajwa tena Agosti 15 mwaka huu.

mwisho

No comments:

Post a Comment