TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 28 July 2011

DPP,Hoseah acheni mchezo wa kuigiza katika jambo zito la vijisenti

Na Mwandishi Wetu

WANAHARAKATI na wachambuzi wa mambo ya siasa nchini wamemtaka Mkuu wa TAKUKURU, Dkt. Hoseah na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Feleshi kuacha mchezo wa kuigiza wa kutupiana mpira bali waoneshe faili la Bw. Andrew Chenge anayetuhumiwa kujilimbikizia dola za kimarekani bilioni moja katika benki ya mjini Jersey, Uingereza.

Profesa Abdallah Safari wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Vunjo, Bw. Augustine Mrema, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia, Mwenyekiti wa APPT Maendeleo Bw. Peter Mziray kwa pamoja wametaka mchezo wa kurushiana mpira katika jambo zito kama hilo uanchwe.

"Itafika wakati watanzania watasema basi na kuingia barabarani kufanya maandamano hiyo baada ya kuvumia bila hatua za kisheria kuchukuliwa, kinaachonekana kama vibaka wanaviziana nani anayetangulia kukwapua"alisema Bw. Mbatia.

No comments:

Post a Comment