TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 2 August 2011

Mpiga picha majira adhaminiwa

Baada ya Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Ilala, kukataa kupokea barua ya pili kwa madai ya kuchelewa, mpiga picha wa majira, Bw. Nyakasagani Masenza amepata dhamana.

Bw. Masenza alipata dhamana jana saa 8 mchana baada wadhamini wake wawili Bw. Peter Mwenda wa Majira na Bw. Richard Mwaikenda wa Jambo Leo kutimiza masharti ya sh. mil. 1 kila mmoja na vitambulisho vya waajiri wao. Kesi ya Bw. Nyakasagani itatajwa tena Agosti 15.

mwisho

No comments:

Post a Comment