Na Peter Mwenda
MKE wa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Dkt. Denise Bucumi Nkurunziza ameishukuru Serikali ya Tanzania kusaidia nchi yake kupata uhuru, kuhifadhi wakimbizi,kusimamia kesi za watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya halaiki na kuwapa uraia wananchi wa nchi yake.
Akizungumza mbele ya mwenyeji wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete juzi, Dkt. Denise Kurunziza alisema amekuja kutoa shukurani kwa watanzania kwa imani yao kusaidia wananchi wa Burundi katika kipindi chote kulipotokea machafuko ya kikabila.
"Nimekuja kutoa shukurani kwa niaba ya wananchi wa Burundi kwa watanzania ambao wamechangia nchi yetu kupata uhuru, kihifadhi wakimbizi wakati wa migogoro ya kikabila na kukubali kuruhusu mahakama ya mauaji ya halaiki kufanyika Tanzania" alisema Dkt. Mkurunziza.
Alisema wananchi wa Burundi wamekuwa wakikimbilia Tanzania wakiamini kupata hifadhi na familia zao katika kipindi chote na wengine wamepewa uraia baada ya kuishi kwa miaka mingi.
Dkt. Kurunziza alisema amerudi kutoa shukurani zake kwa niaba ya wananchi wa Burundi yeye akiwa mmoja wa wao aliyewahi kuishi Tanzania wakati nchi hiyo ikiwa katika machafuko ya kikabila hivyo amerudi kuwashukuru watanzania kupitia Mama Salma Kikwete.
Alisema amefurahishwa kuona Tanzania inavyojitahidi kuleta haki sawa kwa akinamama na kupambana kuondoa tatizo la watoto wa mitaani jitihada ambazo zinafanywa pia nchini Burundi.
Alisema kuna sababu nyingi za kuwepo watoto wa mitaani lakini nchini Burundi Serikali inajitahidi kukabiliana na watoto wa mitaani ambao wengine wanafanya mazoea kuzurura mitaani.
Alisema Serikali inatafuta njia ya kuwatafutia shule wale watoto ambao umri wao ni mdogo na wengine wanatafutiwa kazi japokuwa baadhi yao hawataki kukubali chochote zaidi ya kuzurura hivyo kuipa Serikali wakati mgumu.
Awali mwenyeji wake Mama Kikwete alisema watanzania walijitolea kusaidia mapambano ya kuleta uhuru barani Afrika kwa sababu hakufurahishwa kuona majirani zake wanaotawaliwa na wakoloni.
Alisema hata baada ya kujikomboa Tanzania haikupendezwa kuona kuona raia wa nchi jirani wakiuana kwa sababu za kisiasa na kikabila.
Alisema kutokana na machafuko ya kisiasa kwa nchi jirani iliamua kupokea wakimbizi na kuwatunza hadi waliomaliza migogoro yao.
Mama Kikwete alisema kuhusu mfumo wa kijinsia Tanzania imepiga hatua kuleta uwiano wa wanawake kwa asilimia 40 na kuongeza jitihada za kuondoa kabisa watoto wa mitaani.
mwisho
No comments:
Post a Comment