Na Peter Mwenda
DKT. Sengondo Mvungi ameitaka Serikali kuibunja EWURA na ifutwe kwenye orodha ya taasisi za Serikali kwa sababu haina faida kwa watanzania kwa sababu ndiyo iliyolifikisha taifa katika wakati huu wa kukosa mafuta.
Alisema EWURA ilipaswa kujua wajibu wake kama idara ya Serikali ilipaswa kukaa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC)kuagiza mafuta yasiyosafishwa na kuwauzia wafanyabiashara nchini.
"EWURA inakaa kwenye komputa kuangalia bei ya mafuta na kupanga bei matokeo yake watanzania wanashindwa kuona chombo hicho kinavyoshindwa kuwasaidia na kupandisha mafuta ya taa kwa kisingizio yanaongeza uchakachuaji" alisema Dkt. Mvungi.
Alisema Serikali hii li legelege kwa sababu ishindwa kuwasaidia wananchi wake ambao wameingia kwenye kadhia ambayo wasingeweza kuipata endapo EWURA igejipanga kuondoa matatizo ya mafuta.
"Tazama kama kitu huna uwezo nacho usijiweke kimbelembele lazima kiundwe chombo cha kuchukua nafasi ya UWURA ya kuagiza mafuta na kuuwauzi wafanyabiasha nao wauzie wenye magari" alisema Dkt. Mvungi.
Alisema UWURA iende kuzimu kqwa manuifaa ya watanzania kwa sababu imeshindwa kuonesha kuwepo kwake kuna nini kimefanyika kwa manufaa ya watanzania.
mwisho
No comments:
Post a Comment