Na Peter Mwenda,Kisarawe
MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Bw. Selemani Jafo anaendelea kukuna kichwa kutafuta wafadhili wa kuchimba visima virefu ili kupunguza uhaba mkubwa wa maji katika kata 15 za jimbo hilo.
Akizungumza katika ziara ya kuona matatizo ya maji kwa wananchi wa jimbo hilo akifuatana na Mhandisi wa Maji pamoja na Mafundi Sanifu wa wilaya katika Kata mbalimbali alilakiwa na kero za wananchi wanazopata kuhusu uhaba wa maji.
Wakanchi hao ambao walichangia hoja mbalimbali za kutatua tatizo hilo wananchi wa Kata ya Marui walikutwa wakigombea maji ya mvua yaliyotuwama katika barabara ya Kisarawe kwenda Vikumburu.
"Baba mbunge wetu maji ya shinda kutoka alfajiri tupo hapa tukigombea maji ya mvua,tunatumia muda mrefu kupata maji hatujui mvua zikisimama tutapata wapi maji" walilalamika akinamama hao.
Katika ziara hiyo Mbunge Jafo alikagua bwawa la Vikumburu ambalo ndilo pekee linalotegemewa na wananchi wa kata hiyo na Chole ambalo hata hivyo maji yake yameanza kuzingirwa na magugu maji.
Mbunge hiyo akiwa katika kijiji cha Kisangire kata ya Marui wananchi wake walimuomba awachimbie bwawa la kuhifadhi maji kwa sababu kijiji hicho hakina kisima baada ya kile kilichokuwepo kujaa mchanga na kusababisha maji kushindwa kutoka.
Katika kijiji cha Sofu ambako kunatarajiwa kuchimbwa kisima kirefu, Mbunge huyo alisema wananchi wakae tayari kupokea mradi huo na kusaidia ujenzi wa kisima hicho.
Bw. Jafo akizungumzia uhaba wa maji alikiri kuwa jimbo lake linakabiliwa na uhaba mkubwa na ndiyo shida inayoongoza na kumuumiza kichwa.
mwisho.
No comments:
Post a Comment