TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 11 May 2011

Damu Salama kuzindua kituo Mnazi Mmoja

Na Peter Mwenda

MPANGO wa Taifa wa Damu Salama Tanzania,kesho unazindua kituo kidogo cha kuchangia damu katika hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Rajabu Mwenda alisema kituo hicho ambacho kitakuwa cha tatu nchioni kitakuwa na uwezo wa kukusanya zaidi ya lita 20 za damu.

Alisema lengo la kufungua kituo hicho ni kusogea karibu na watu wenye nia ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao wanaohitaji huduma ya damu katika hospitali mbalimbali nchini.

Bw. Mwenda alisema kituo hicho ni cha tatu baada ya Makao Makuu na kingine Kanda ya Mashariki vilivyoko Mchikichini,vingine vinatarajiwa kufunguliwa mwezi Juni mwaka huu mjini Dodoma na baadaye kingine katika mkoa wa Lindi.

Alisema katika hafla ya uzinduzi wa kituo hicho mgeni rasmi atakuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Margareth Mhando.

No comments:

Post a Comment