Na Peter Mwenda
MWANAFUNZI wa kidato cha Pili wa shule ya bweni ya Image mkoani Iringa, Lawrance Aron Hongoa (14) ametoweka na kwenda mahali pasipojulikana wakati akienda shuleni kutoka likizo kwa wazazi wake.
Baba wa mwanafunzi huyo, Bw.Aron Hongoa akizungumza katika ofisi za majira jana alisema mwanaye aliondoka Aprili 21 nyumbani kwa baba yake mdogo Bw. Hongoa Kiseki mjini Iringa kwenda shuleni lakini hakufika.
Alisema mwanaye alianza safari ya kwenda shuleni Aprili 19 mjini Dar es Salaam ambako ndiko anaishi na mama yake kumsindikiza kupanda basi la kwenda Iringa ambako alifikia kwa baba yake mdogo.
Baada ya kufika Iringa alipumzika siku moja na siku iliyofuata alipanda basi la kwenda shuleni Image ambako hakufika hadi sasa.
Bw. Hongoa alisema jitahada za kumtafuta mwanaye kumshirikisha baba yake mdogo, walimu na familia yake ya Dar es Salaam katika vituo vya polisi na hospitali zote bila mafanikio.
Alisema walitoa ripoti katika kituo kikuu cha polisi mkoa wa Iringa kwa jalada namba IR/RB/2486/11 ya Mei 5, mwaka huu na kuwataka wananchi watakaomuona watoe taarifa kituo chochote cha polisi na kuwasiliana naye kwa namba 0715 666355,0752 353063, 0718 425539,0713 600285.
mwisho
No comments:
Post a Comment