TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 20 May 2011

Shekhe Yahya Hussein afariki dunia

MNAJIBU na Mtabiri mkuu nchini,  Sheikh Yahya Hussein amefariki leo Ijumaa nyumbani kwake Magomeni Dar es Salaam.
   Taarifa iliyotolewa na Shekhe Mkuu, Mufti Shaaban Bin Simba alisema taaratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake.
   Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-salaam.
    Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo kilichojulikana kama Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo.
    Baada ya kuhitimu alikwenda nchini Misri alipoendelea kusomea masuala ya dini katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.
   Alirejea nchini mnamo miaka ya mwanzoni ya 60 ambapo alianza kazi yake ya utabiri . Sheikh Yahya Hussein ndiye mtabiri wa mwanzo kueneza utabiri wa kila siku katika magazeti mbalimbali ya Afrika Mashariki enzi hizo.
   Jina lake lilivuma zaidi alipokuwa akitoa utabiri kupitia radio kuhusu mashindano ya mpira kati ya nchi tatu za Africa Mashariki yaliyojulikana kwa jina la Challenge Cup au Gossage Cup.


Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi....

No comments:

Post a Comment