Na Peter Mwenda
PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kitunda,Dar es Salaam Padre James Mweyunge ameongoza viongozi wa Baraza la walei wa Parokia hiyo kutoa misaada kwa watoto yatima na wazee wasiojiweza wa kituo cha Msimbazi ikiwa ni maadhimisho ya Kanisa hilo la Roho Mtakatifu yanayofanyika Jumapili Juni 12,2011.
Akizungumza katika mahabusu ya watoto ya Kisutu, Padre Mweyunge aliwaaasa watoto hao kuacha tabia ya utukutu na kubadilisha tabia zao ili kwani kwa kufanya hivyo wanatakuwa vijana wazuri katika jamii.
"Viongozi wengi duniani ambao wamekuwa marais waliwahi kufungwa gerezani na nyinyi msikate tamaa, badilikeni kwani mnaweza kuwa wabunge na marais hapo baadaye"alisema Padre Mweyunge.
Katibu wa Parokia hiyo, Bw. Saimon Nguka alisema msaada uliokabidhiwa katika vituo hivyo ni mafuta ya kupikia, mchele, sabuni,magodoro,viatu, juisi, biskuti,maji,sukari na maziwa ya kopo.
mwisho
No comments:
Post a Comment