Na Mwandishi Wetu
JUMUIYA ya watu walio katika imani za Kirastafarian nchini,TARAMO kimeandaa tamasha maalum la kukumbuka siku kuzikwa kwa mwasisi wa mindoko ya muziki wa Raggae Ulimwenguni,Nesta Robert Marley, maarufu kama 'Bob Marley' lililopangwa kufanyika Jumamosi ya Mei 21 mwaka huu katika ufukwe wa Hunter's, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hayati Bob Marley alifariki dunia Mei 11, mwaka 1981 na kuzikwa Mei 21 ya mwaka huo nchini Jamaica, ambapo chanzo cha kifo chake kilitokana na ugonjwa wa kansa ya kidole gumba cha mguu iliyosambaa mwilini.
Mwenyekiti wa chama hicho, Ras Bumija alisema jana kuwa tamasha hilo litafanyika kuanzia saa sita mchana na kuendelea mpaka usiku wa manane na kusindikizwa na burudani mbalimbali za muziki wa reggae utakaopigwa 'laivu' na wanamuziki wa miondoko hiyo nchini.
Alizitaja bendi hizo ni pamoja na Afrikabisa inayoongozwa na mkongwe wa muziki wa reggae nchini Jikho Man pamoja na Machifu Band iliyo chini ya Ras Gwandumi.
Ras Bumija alizitaja burudani zingine zitakazosindikiza tamasha hilo zitatumbuizwa na washindi wa mashindano ya Tuzo za Kilimanjaro kwa mwaka 2011, Hard Mad pamoja na Mzungu Kichaa wa BSS.
Alisema,Hard Mad amealikwa ili aweze kuwatumbuiza washabiki wamuziki wa reggae na sambamba na kuwashukuru kwa kumpigia kura zilizomwezesha kunyakuwa tuzo ya muziki wa Reggae mwaka 2011.
Aliongeza Ras Bumija kuwa, Mzungu Kichaa ameingizwa katika ratibaya burudani kutokana na mchango wake katika fani ya muziki wakizazi kipya nchini unaopendwa na marika yote nchini kutokana na ukweli kuwa, onyesho hilo itahudhuriwa na watu wa marikambalimbali.
"Tumepanga kuwashirikisha wasanii wengi kwa ajili ya kuongezamaana ya onyesho lenyewe likalohusisha pia maonyesho na mauzo ya mavazi ya asili ya Afrika na vyakula vya asili ya bara hili la watu weusi ambapo kiingilio kimeapangwa kuwa shilingi elfu tatu ili kuweza kuwapa fursa washabiki wengi wa muziki nchini kuhudhuria" alisema Ras Bumija na kuongeza.
"Tukiwa miongoni mwa wafuasi wa imani za Kirastafari tuishio Tanzania tumeliingiza tukio la siku ya kuzikwa kwa hayati Bob marley katika kalenda ya matukio yetu ya mwaka ambayo huyaazimisha na kuyakumbuka kwa kushiriki mikusanyiko ya shughuli za kijamii pamoja na burudani za kuenzi kazi za mwasisi wa reggae ulimwenguni".
Alitoa wito kwa washabiki wa muziki na burudani kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo la Kigamboni,kwani litatimiza kumbukumbu ya kweli na ya pamoja kwa jamii ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment