Taasisi ya Keko Mwanga Development Foundation (KEMWADEFO) imeandaa hafla ya kutoa mipira kwa timu 10 zitakazoshiriki mashindano ya kumuenzi muasisi wa soka katika eneo la Keko Mwanga jijini Dar es Salaam.
Katibu wa KEMWADEFO, Peter Mwenda amesema mipira hiyo yenye thamani ya sh.450,000 imetoalewa na taasisi yake kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kabla ya mashindano ya Kizoka Cup kuanza Januari 15 mwaka huu.
Lengo kubwa na taasisi hiyo ni kuwaweka vijana pamoja na kuwaepusha na vishawishi vya kuingia katika mambo yasiyofaa katika jamii kama kuvuta bangi, ulevi na unyang'anyi.
Mjumbe wa Temeke Abbas Mtemvu ndiye atakayekuwa mgeni rasmi na wanahabari na wadau wa michezo wanakaribishwa kuhudhuria.
No comments:
Post a Comment