TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 18 December 2010

Chuo cha Ufundi Bruno kujenga mabweni ya wasichana

Na Peter Mwenda

CHUO cha Mafunzo ya Ufundi Bruno  (BVTC) kinajenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike toto wa kike ili kutoa elimu ya ufundi sambamba na wanaume.
Mkurugenzi Mtendaji wa BVTC, Bw. Bruno Ndege akizungumza katika mahafali ya 16 ya chuo hicho Bw. Bruno alisema kwa kuanzia yatajengwa mabweni mawili katika eneo la chuo na kuongeza mengine endapo eneo la kutosha litapatikana.

"Bodi wa wadhamini wa Chuo wameazimia kujenga mabweni kwa ajili ya watoto wa kike wapate nafasi ya kutosha kujifunza masomo ya ufundi kwa sababu wanawake wakiwezeshwa wanaweza" alisema Bw. Ndege.

Katika mahafali hayo ambayo yalijumuisha Chuo cha BVTC cha Malapa na chuo cha Pugu Mwakanga, mgeni rasmi Bw. Justine Nyangwe aliyemwakilisha Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela alianzisha harambee wa kuchagia mabweni hayo na wazazi kuchangia na wengine kuahidi kutoa ushirikiano kwa chuo hicho.

Awali risala ya wanachuo hao ilisema maendeleo ya chuo hicho kitaaluma yanazidi kuwa mazuri na kutoa changamoto kwa wazazi kuwapeleka watoto wao kusomea ufundi kwa sababu hiyo ni ajira inayojitosheleza.

Ilisema mafundi wa magari waliopo jijini Dar es Salaam ni matunda ya chuo hicho katika fani za umeme wa magari, usukaji mota, na mashine mbalimbali,unyoshaji bodi na udereva wengi wao wamesoma chuo hicho.

Wanachuo hao walisema changamoto zinazokikabili chuo hicho upungufu wa vifaa vya kufundishia kwa vitengo kama injini za magari, kabureta, mitungi ya gesi ya kutosha ya kuchomea bodi na kupatikana eneo la kutosha la kupanua.

Awali Bw. Ndege alisema kati ya wanachuo 104 waliomaliza mafunzo ya ufundi juzi wawili ni wa kike ambao wanaweza kufungua na kufunga injini za gari aina yoyote.

Alisema kutokana na mafanikio hayo chuo hicho kimeamua kutoa upendeleo kwa wanafunzi wa kike ili wajifunze ufundi na wakimalizawatapewa nafasi ya kwanza kutafutiwa kazi.

Bw. Ndege alisema matarajiocha chuo hicho ni kuwa kitovu cha elimu ya ufundi kitakachosaidia kuwakwamua vijana wasibweteke vijiweni na badala yake wazalishe mali manufaa ya familia zao na taifa.
mwisho.

No comments:

Post a Comment