TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 22 October 2010

Wanafunzi shule 12 za msingi kufundishwa' utrafiki' Dar

Na Peter Mwenda

KIKOSI cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini kimeandaa mafunzo kwa wanafunzi wa shule 12 za mkoa wa Dar es Salaam jinsi ya kuvusha wenzao wanapokwenda au kurudi kutoka shuleni unaojulikana kama Junior Patrol.

Kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani Nchini, Bw. Mohamed Mpinga aliambia Mwendablog kuwa mafunzo hayo yatafanyika katika shule zinazopakana na barabara kuu za Jiji la Dar es Salaam.

Shule hizo ni Mbuyuni (Oysterbay),Kumbukumbu (Morocco), Minazi Mirefu (Ukonga), Lumumba, Bunge, Kasulu, Msimbazi na Dkt. Omari za wilaya ya Kinondoni. Miburani, Kibasila, Muungano na Mtongani wilaya ya Temeke.

Wanafunzi wawili watasimama pembeni mwa barabara wakiwa wamevaa jaketi zenye kuaksi mwanga (reflaction) na kibao chenye kuonyesha Nenda na upande wa pili Simama.

Mafunzo hayo ni ya nchi nzima na Kamanda amesisitiza kuwa lengo ni kuondoa vifo vya watoto chini ya miaka 19 ambao katika takwimu za Januari hadi Septemba 2010 watoto  wapatao 496 walikufa kwa kugongwa na magari na kujeruhi 2,623.

No comments:

Post a Comment