TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday 31 August 2010

Wananchi waua majambazi Dar,bomu lajeruhi watoto Bagamoyo

Na Peter Mwenda, Polisi



WANANCHI wenye hasira kali wamewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa silaha za jadi na kisha kuwachoma moto eneo la Mbezi Makonde, Dar es Salaam leo saa 5 asubuhi.

Majambazi hayo yaliyokuwa zaidi ya tisa yalivamia nyumba ya Adam Nyangasa (52) na kumkuta msichana aliyewakaribisha baada ya kujifanya wageni wa nyumba hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,Bw. Elias Kalinga anaeleza kuwa majambazi hayo yalimlazimisha msichana huyo kufungua mlango na kuingia ndani ambako waliiba laptop.

Katika harakati za kutoroka wananchi walisikia kelele za msichana huyo ndipo ulipogeuka uwanja wa vita risasi ziliporindima kutoka kwa majambazi hao na wananchi kujibu mashambulizi kwa njia ya kujihami kufuatia elimu ya ulinzi Shirikishi katika jamii.

Katika tukio jingine mwanafunzi Salum Mohamed (14) wa shule ya Rajab Ramadhani(16)wakati wakiwinda ndege na kuokota kitu mfano wa bomu kilichowalipukia na kuwajeruhi vibaya sehemu mbalimbali za mwili.

No comments:

Post a Comment