TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday 2 May 2016

Uswahilini waibuka mabingwa wa Mama Shija

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Soka ya Uswahilini FC imeibuka mabingwa wa Kombe la Mama Shija baada ya kuichapa Wamangati zote za Mbagala katika fainali ilijaa ushindani mkubwa iliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kingunge, Mbagala Dar es Salaam.
Katika fainali hizo ambazo zilidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Vodacoma, mshambuliaji Sultani Kasikasi wa Uswahilini aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuifungia timu yake mabao 3 yaliyoipatia timu yake ubingwa na kuzawadiwa mpira "hat Trick".
Mabao ya Kasikasi yalipatikana dakika ya 32 , dakika ya 41 na 59 na mabao ya WAmangati yaliyungwa na Salum Gava dakika ya 39 na bao la pili lilifungwa na Musa Madebe aliyeunganisha krosi safi ya Shaaban Pazi.
Muandaaji wa mashindano hayo, Fatuma Shija akizipongeza timu zote 20 zilizoshiriki Kombe hilo aliwataka vijana kutumia muda wao mwingi kwenye michezo ambayo itachukua muda wao mwingi kujenga miili yao badala ya kuvuta bangi na kufanya vitendo vya kihuni mitaani.
Mashindano hayo yalishirikisha timu kuoka Mkuranga mkoa wa Pwani, Wilaya Mpya ya Kigamboni na Temeke, Mshindi wa nne ilikuwa timu ya  Kisemvule FC iliyezawadiwa mpira mmoja, mshindi wa tatu ni Bodabdoda iliyopata  jezi seti moja na mpira mmoja na mshindi wa pili alipata medali 15 za shaba, jezi seti mbili na mpira mmoja.
Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Uswahili baada ya kuzawadiwa Kombe na medali 15 za dhahabu kwa wachezaji wake, jezi seti mbili na mpira mmoja walishangilia na kucheza uwanja mzima  huku kuimba nyimbo za ushindi na kuwavutia mashabiki wake na wapita njia.
mwisho

.

No comments:

Post a Comment