TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday 5 May 2016

Timu ya mchezo wa mpira wa Roll kuwakilisha Tanzania Kenya



Na Peter Mwenda

TIMU ya Taifa ya Mchezo wa mpira wa kuteleza(Roll Ball) imeondoka jana ikiwa na wachezaji 12 kwenda Kenya kwenye mashindano ya kimataifa ya Afrika yatakayoanza leo mjini Nairobi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo,Arthur Haule alisema jana Dar es Salaam kuwa wamejiandaa kutwaa ubingwa wa mchezo huo utakaoshirikisha timu kutoka mikoa sita.

Alisema safari yao ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Nadia House of Beuty inaondoka na wachezaji 12 na viongozi wawili.

Aliwataja wachezaji watakaowakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ni Mohammed Athumani, Emmanuel Thomas, Hamisi Salum, Rajab Kassim, Omari Madohola, Yakhe Shaaban,Jonas Emmanuel, Fahadi Waziri, Said Abdallah,Kassim Rajab, Feruzi Juma na Clement Andrea.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty, Nadia Azmat akikabidhi vifaa vya michezo kwa safari hiyo aliwataka watanzania wengine kusadia michezo ambayo haina umaarufu ili kuibua vipaji mbalimbali vya vijana.

Nchi zinazoshiriki mashindanoi hayo ni wenyeji Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia.


mwisho


No comments:

Post a Comment