Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
MKUU
wa Wilaya ya Mkuranga, Abdallah Kihato amewataka wasanii kuacha tabia
ya kukata tamaa kuwa wao ni masikini kwa vile vipaji walivyonavyo
wakivitumia vizuri ni utajiri mkubwa katika maisha yao.
Akizungumza
katika sherehe za kukabidhi nyumba 25 za wasanii wa kijiji cha
Mwanzega, Mkuranga mkuu huyo wa wilaya alisema wasanii wamekuwa
wakijiiita masikini lakini ukweli ni kwamba vipaji walivyonayo ni
utajiri mkubwa kwao na taifa zima.
Alisema vipaji
walivyonavyo vya kuelimisha jamii kutumia sanaa na kuburudisha ni
utajiri ambao kama utatumiwa vizuri hakuna msanii atakayejiona masikini
mbele ya jamii.
"Mimi ni mwamuzi wa soka niliyesomea kazi
hiyo pia ni msanii mwenzenu ninayefuatilia kazi za sanaa za kila siku za
watanzania, nimewahi kufanya mengi katika sanaa pia niliwahi kuchezesha
mechi ya Simba na Yanga kwenye uwanja wa Karume miaka ya zamani lakini
purukushani zake zilifanya nisichezeshe tena" alisema Mkuu wa Wilaya
Kihato.
Alisema kijiji cha Wasanii Mwanzega kina kiloa sifa
za kukifanya kiwe cha nyumba za asili kama kivutio cha watalii kutoka
nje ya nchi na kuwataka viongozi wa SHIWATA kuandaa tamasha kubwa la
wasanii wa fani zote kijijini Mwanzega.
Kihato alisema
Serikali iko tayari kutoa mchango wake katika tamasha hilo ambalo
alisema kama likitangazwa vizuri wasanii na watanzamaji kutoka sehemu
mbalimbali za dunia watafika kijijini kuhudhuria na kuona vivutio
vilivyopo.
Mkuu huyo alisema amesikia kilio cha wanakijiji
hao cha kuomba wapatiwe umeme, maji na barabara na kuahidi kuwa Serikali
iko tayari kutekeleza hilo kama wasanii na wanakijiji wa Mwanzega
watawasilisha maombi yao.
Awali Mwenyekiti wa SHIWATA,
Cassim Taalib alisema kijiji wasanii Mwanzega mpaka sasa kimekwisha
kujenga nyumba 150 kwa njia yawanachama kujichangisha.
Katika
sherehe hizo zilizosindikizwa na burudani ya kikundi cha matarumbeta
cha eEbeneza cha Manzese, Dar es Salaam, wachezaji maarufu wa zamani wa
Yanga, Salvatory Edward na Kipa HAmisi Kinye walikabidhiwa nyumba zao.
Wasanii
wengine waliohudhuria sherehe hizi ni Kikundi cha Tanzania One Theatre
(TOT) wakiongozwa na Ali Stars na Abdul Misambano ambao nao waliahidi
kuanza ujenzi kwa njia ya kuchangishana katika kijiji hicho.
SHIWATA
yenye wanachama zaidi ya 8,300 inamiliki hekari 300 za kujenga nyumba
za makazi katika kijiji cha Mwanzega na hekari 500 za kulima mazao
mbalimbali katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga mkoani Pwani.
mwisho
No comments:
Post a Comment