TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday 25 July 2015

Wananchi wakumbwa na suasua ya kujiandikisha kupiga kura

Na Mwandishi Wetu


WANANCHI kutoka vituo mbalimbali vya kujiandikisha kupata vitambulisho vya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba 2015 wameingiwa na wasiwasi kuhusu kasi ndogo ya uandikishaji wapiga kura kutokana na sababu zinazodaiwa kuwa mashine maalum za BVR nyingi hazifanyi kazi.

Mmoja ya vituo hivyo ni cha Sokoni, Kivule Kitunda ambako mpaka jana watu waliojiorodhesha kwenye daftari ili kupewa namba ambazo wamepangiwa siku ya kuandikishwa na kupewa vitambulisho inawatisha.

Kutoka kazi ya uandikishaji ianze Julai 22 mwaka huu katika kituo hicho wananchi 100 pekee wamekabidhiwa vitambulisho kati ya 2200 waliojiandikisha hadi jana asubuhi.

Diwani wa Kata ya Kivule, Nyansika Getama akizungumza katika kituo hicho alisema kasi hiyo ni ndogo ambayo inawafanya wananchi wachanganyikiwe na wengine kukata tamaa.

Mwandishi na mtangazaji wa TBC, Jesse John ambaye alifika kujiandikisha alijikuta anakuwa mtu wa 2115 na kupewa siku ya Ijumaa ijayo afike kujiandikisha na kupewa kitambulisho.

Kituo hicho hakina tofauti na vituo vingine vya Ilala Bungoni, Banana, Kitunda na vingine ambavyo malalamiko yanazidi kuongezeka siku hadi siku.

 


mwisho

No comments:

Post a Comment