TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 31 July 2015

Tumeini muda wa nyongeza kujiandikisha BVR

Na Peter Mwenda

KUJITOKEZA kwa wingi kwa wananchi kujiandikisha kupiga kura ni hatua moja mbele ya kujivunia ili kujenga demokrasia ya kuchagua viongozi wanaofaa kwa maendeleo ya nchi.

Kutoka kazi ya uandikishaji ianze mapema mwaka huu kutumia mashine za kisasa za kieletroniki za (BVR)idadi ya waliokwisha jiandikisha mpaka sasa ni mil.18 nchini kati ya mil. 24 wanaotarajiwa kuandikishwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini(NEC) Jaji mstaafu Damian Lubuva na tume yake wameongeza siku nne zaidi kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakikesha vituoni kujiandikisha lakini hawafanikiwi.

Sababu kubwa iliyozorotesha uandikishaji katika daftari la kudumu la Wapigakura kutumia mfumo wa BVR katika mkoa wa Dar es Salaam ni nyingi, chache ya hizo ni mashine nyingi kushindwa kusoma, wataalamu wake kushindwa kutumia mashine hizo na utaratibu mbovu wa kupanga foleni.

Nimewahi kutembelea vituo vingi kutoka kazi ya uandikishaji na utoaji vitambulisho vya kupigia kura ianze mapema mwaka huu katika mkoa wa Dar es Salaam wafanyakazi wengi wameshindwa kupata vitambulisho hasa kutokana na muda wa kazi.

Nakubali kuna ukiukwaji wa uandikishaji kwa sababu baada ya kuonekana muda hautoshi wengine walijiandikisha kwenye vituo karibu na sehemu zao za kazi ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kumpigia kura kiongozi wanaomtaka.

Kabla ya NEC kuongeza siku nne za kuandikisha kwenye daftari la Kudumu la Wapigakura wananchi,wengi walikata tamaa ya kujiandikisha nikiwemo mimi.

Katika kituo changu cha kujiandikisha nilikuwa daftari likiwa na orosha ya watu 2,100 wakati huo waliojiandikisha ni watu 300 ikiwa siku ya tatu kutoka kazi ya uandikishaji ianze.

Nilipangiwa kurudi Ijumaa ambayo ilikuwa siku ya mwisho na nilipofika nikaambiwa utaratibu umevurugika na kuanza upya uandikishaji na hiyo ni katika siku nne zilizoongezwa.

Wasimamizi wa kituo changu walijaribu kuweka makundi ya watu wanaohitaji msaada kama walemavu, wazee na akinamama wajawazito lakini hiyo ilipingwa na watu wengine,

Kuna baadhi ya vituo wasimamizi kutoka serikali za mitaa walibuni utaratibu wa kupanga foleni kwa kujiandikisha ili zamu ikifika akajiandikishe na wengine aliyewahi ndiye aandikishwe.

Utaratibu huo ulitumiwa katika vituo vingi lakini kasi ya kujiandikisha iliongezeka siku hadi siku na hasa baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kutangaza kuhamia CHADEMA.

Sijui kundi la waliojitokeza dakika za mwisho kujiandikisha wamepataje morari huo au nini kimewasukuma mpaka kujiandikisha wakati wengi waliapa hawatapiga kura.

Hata hivyo naungana na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lubuva wakati akiongeza siku za kujiandikisha kwa mkoa wa Dar es Salaam kuwa wameongea muda zaidi kwa sababu wananchi wengi wamejitokeza muda wa lala salama.

"Uamuzi wa kuongeza muda wa kujiandikisha kupiga kura umetokana na mwamko mkubwa wa wananchi wanaojitokeza kujiandikisha katika vituo mbalimbali" alisema Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lubuva.

Siku nne si nyingi kulingana na umati mkubwa wa wananchi ambao bado wanasota vituoni kutoka alfajiri mwaka vituo vinafungwa bila kuonja chochote mdomoni wala kufanikiwa kujiandikisha.

Wito wangu kwa NEC ni kwamba wasiwasubirie watendaji wa Halmashauri za Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke kuwasilisha ripoti ya kuongeza mashine za kuandikisha au kuharibika kwa mashine hizo.

NEC iingize nguvu zake katika mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwatuma kikosi kazi ambacho kitatembelea kila kituo na kurekebisha kasoro zinazojitokeza kuliko kusubiri watendaji wa Halmashauri.

Mbali ya wito alioutoa Mwenyekiti wa NEC wa kuhamasisha wengine kujitokeza kujiandikisha natumia nafasi hiyo pia kuwaomba vijana, wazee na hata wale ambao walitaka mgombea fulani wa nafasi ya Urais wa nchi lakini hakupitishwa wajiandikishe.

Jambo jingine ambalo sisi tuliobaki kujiandikisha katika mkoa wa Dar es Salaam tuwe makini na wahamiaji haramu ambao wanajiandikisha nchini kwetu.

Mpaka sasa raia wa kigeni 2,048 kutoka nchi jirani ambao wamejiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura ili kujipatia vitambulisho waonekani ni watanzania.

Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji nchini, Abbas Irovya alisema raia hao wametenda kosa na wamerudishwa makwao na wengine kuchukuliwa hatua za kisheria.

Petermwenda0@gmail.com 0715 222677






No comments:

Post a Comment