TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday 21 January 2015

Sherehe za kukabidhi nyumba za SHIWATA Mkuranga

NYUMBA 40 zimekabidhiwa kwa wasanii, wanahabari na wanamichezo waliokamilisha michango ya kuchangia ujenzi wa nyumba za wasanii zinazoendelea kujengwa katika katika kijiji cha wasanii, Mwanzega Mkuranga mkoa wa Pwani.

Kati ya wanamichezo waliokabidhiwa nyumba hizo ni mama wa aliyekuwa  mcheza filamu maarufu marehemu, Steven Kanumba aliyekabidhiwa banda lenye thamani ya sh. 631,000.

Mwamamichezo mwingine, Fabian Makolo ambaye aliwahi kuchezea timu ya Ashanti,Mwanga All Stars na timu nyingine za Jeshi la Polisi Makao Makuu aliwashukuru viongozi wa Mtandao wa Wasanii Tanzania SHIWATA kwa kazi hiyo.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema sherehe rasmi za kukabidhi nyumba hizo zitafanyika Juni mwaka huu ambako kutakuwa na michezo mbalimbali ya soka, netiboli, maigizo, sarakasi na taarab.

mwisho

No comments:

Post a Comment