Na Peter Mwenda
MTANDAO
wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) imeandaa tamasha kubwa la kuadhimisha
miaka kumi (10) kutoka uanzishwe mwaka 2004 kwa michezo mbalimbali
ukiwemo mpambano wa maveterani wa watani wa jadi Simba na Yanga litakalofanyika kilele cha sherehe hizo uwanja wa Karume,Dar es Salaam Desemba 25,(Krismasi) mwaka huu.
Alisema
ili kuwavutia wenye nyumba hizo wahamie kijijini, SHIWATA imetoa eneo
maalumu kwa ajili ya kulima bustani ya mboga mboga na mazao ambayo si ya
kudumu ili wajikimu wao wenyewe na familia zinazowazunguka.
Alisema
SHIWATA unaomiliki shamba la ekari 500 katika kijiji cha Ngarambe,
Mkuranga unasimamia usafishaji wa shamba hilo kutumia mtambo wa kisasa
(bulldozer) lililokodishwa kutoka Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya
Dar es Salaam kwa gharama ya sh. mil. 22 kwa siku 20 kukamilisha kazi
hiyo.
Alisema Bulldozer hilo limefikisha siku kumi sasa kutoka kazi ya kusafisha shamba hilo na kung’oa visiki ianze,
wanachama 90 waliomilikishwa sehemu ya shamba kwa lengo la kulima mazao
yanayostawi eneo hilo, wameanza kuchangia gharama za kusafisha shamba
hilo.
Mwenyekiti
huyo alisema mazao yanayostawi eneo hilo ni mpunga, mahindi, mbaazi,
viazi vitamu, ndizi, kunde, korosho, mtama na matunda kama embe,
machungwa, matikiti maji na mafenesi.
Alisema
pia kuwa sherehe za maadhimisho hayo zitawakutanisha wakongwe wa soka
wa Simba na Yanga ambao ni wanachama wa SHIWATA wamekubali kushiriki
mpambano huo.
Kwa
upande wa Yanga, mchezaji wa zamani wa Klabu hiyo, Mtwa Kiwhelo na
Athumani Juma Chama kwa upande wa Simba wanawawakilisha wenzao katika
maandalizi ya awali ya mchezo huo.
SHIWATA
yenye wanachama zaidi ya 8,000 kutoka fani mbalimbali za sanaa za
maigizo, mpira wa miguu, mpira wa wavu, netiboli, waigizai wa filamu,
muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, vijana na waandishi wa Habari
kila kundi litapewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao siku hiyo.
mwisho
Details
|
105 more
Show details
|
TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION
TANGAZO SHIWATA
Monday, 17 November 2014
SHIWATA yaandaa tamasha kamambe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment