Na Peter Mwenda
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama Tanzania kushirikiana na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ)umevuka lengo na kukusanya chupa za damu kwa asilimia 97% katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba 2014.
Ofisa uhusiano wa Mpango wa Damu Salama Tanzania, Rajab Mwenda alisema jana Dar es Salaam kuwa katika kipindi hicho jumla ya chupa 34,091 za damu zilikusanywa lengo likiwa chupa 35,000.
Alisema mchanganuo huo unaonesha kuwa vituo vidogo zilikusanywa chupa 2,886, kituo cha Morogoro chupa 1,158, Dodoma 818,M/moja 490, kigoma 93 na Lindi chupa 327.
Alisema wachangia damu wa kujirudia walitoa damu chupa 2,386 na wachangia damu wa mara ya kwanza walichangia asilimia 93 hivyo jitihada zinahitajika kuongeza idadi ya wachangia damu wa kujirudia kwani ndio wachangia damu walio salama.
Alisema jumla ya chupa 10,464 zilitengenezwa mazao ya damu na kusambazwa katika hospitali 212 nchini zenye uwezo wa kutoa huduma ya damu.
Alisema wachangia damu 17,747 walijulishwa majibu yao baada ya kuchangia damu lengo lilikuwa ni kufikia asilimia 70 ya wachangia damu.
Mpango wa Taifa wa Damu salama umefungua kituo kidogo cha kukusanya na kusambaza damu mkoani Kigoma, kituo ambacho kitakuwa na uwezo wa kukusanya chupa angalau 5,000 kwa mwaka.
Pamoja na mafanikio ya kuongezeka kwa wachangia damu kumekuwepo na changamoto mbalimbali za mahitaji makubwa ya damu kuliko upatikanaji,uelewa mdogo wa jamii kuhusu suala zima la uchangiaji damu kwa hiari na uzwaji wa damu usio halali mahospitalini, tabia inayofanywa na watumishi wasio waaminifu.
Changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti ambao unasababisha Mpango kutotekeleza baadhi ya mikakati, upatikanaji wa vitendanishi ambao unaweza sababisha upungufu wa damu hospitalini.
Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeweka mikakati ya kundelea kushirikiana na Taasisi za dini kutoa elimu na kuhamasisha waumini wachangie damu,kama vile
Jumuiya ya madhehebu ya Shia ilichangia damu chupa 900 na jitihada zinafanyika kuhamasisha madhehebu mengine kipindi wanafunzi wa sekondari watakapo kuwa likizo katikati ya Novemba mpaka Januari 2015.
Alisema kila Desemba 6 kila mwaka kutakuwa na siku maalum ya kuchangia damu kwenye
vituo vikubwa vya damu salama toka kwa wanachama wa klabu ya wachangia damu, lengo ni kukusanya chupa 1,800.
'Tutafanya kampeni ya kuhamasisha wananchi kuchangia damu wakati wa siku ya ukimwi duniani Desemba Mosi na siku nyingine zitakazo fuata' alisema Rajab.
Kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali Puplic private partnership (PPP) katika shughuli za kuchangia damu.
Aliwaomba viongozi wa mkoa kupitia mganga mkuu wa mkoa ili wilaya zitenge bajeti ya kukusanya damu, kuelimisha na kuhamasisha jamii nje ya shule na vyuo umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari na kusimamia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu kwa wachangia damu.
mwisho
No comments:
Post a Comment