Kamishina
Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP) Simon Sirro akizungumza
kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa makamanda wa Jeshi hilo
nchini, mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UNDP yana lengo la kuwajengea
uwezo makamanda jinsi ya kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani
bila kuleta madhara makubwa kwa jamii. Kushoto ni Mtaalamu wa Uchaguzi
kutoka UNDP, William Hogan na kulia ni wakufunzi kutoka Uingereza,
Adrian Barnes (kulia) na Alan Binks (wa pili kulia).
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
JESHI
LA POLISI nchini limejisifu kwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi
yao kwa kuruhusu maandamano mengi kufanyika hapa nchini na ni maandamano
machache tu yaliyowahi kupigwa marufuku. MOblog inaripoti.
Akizungumza
na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati
akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa maofisa 88 wa Jeshi la Polisi
yanayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo
(UNDP) kupitia mradi wa Uwezeshaji Demokrasia (DEP), Kamishina
Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon Sirro amesema mafunzo
hayo kwa makamanda ni kusaidia uelewa wao katika kupambana na
maandamano au dalili za uvunjifu wa amani bila kuleta madhara makubwa
kwa jamii.
“mafunzo
haya kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini litasaidia kuongeza uelewa
kuhusu haki za binadamu na utawala bora ili kudumisha amani na utulivu
nyakati za uchaguzi,” amesema Sirro.
Mtaalamu
wa Uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan akizungumza kwenye ufunguzi wa
mafunzo hayo kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu mafunzo hayo
na muhimu wake katika kudumisha amani na kusaidia uchaguzi kufanyika
katika hali ya utulivu na kidemokrasia zaidi.
Kamanda
Sirro amesema kwamba mafunzo hayo yanalenga pia kusaidia uelewa
makamanda jinsi ya kushughulika na wavunjifu wa amani kwa kuzingati
weledi wa Jeshi la Polisi nchini.
Amesema
kuelekea katika uchaguzi mkuu mwakani 2015 mafunzo yamekuja wakati
mwafaka kwa Jeshi la Polisi kupanua wigo wao katika maswala haya ya
utawala bora na haki za binadamu nchini.
“utafiti
unaonyesha kwamba maandamano mengi yamewahi kuruhusiwa na Jeshi la
Polisi kuzidi yale yaliyopigwa marufuku kwa hiyo yana ya kwamba jeshi
linazuia haki za raia kukusanyika au kuandamana haipo isipokuwa kwa
sababu za kiusalama tu,’ aliongeza Kamanda Sirro
Kwa
upande wake, Mtaalamu wa Uchaguzi, kutoka UNDP, William Hogan amesema
kuwa mafunzo hayo yanahusu kumudu kuleta utulivu wa umma na yanaendeshwa
katika ukumbi wa maofisa wa Polisi wa Oysterbay na ukumbi wa maofisa w
Polisi Zanzibar.
Baadhi
ya Maafisa wa Kikosi cha kutuliza ghasia nchini (FFU) nchini
wakifuatilia hotuba za Kamanda Sirro wakati ufunguzi wa mkutano huo
jijini Dar es Salaam.
Amesema
lengo la mafunzo hayo ni kujenga uwezo wa makamanda wa polisi wa
kupanga, kumudu na kuratibu kwa ufanisi hatua za kipolisi za
kushughulikia matukio yanayotishia utulivu katika jamii.
“kupitia
program hii ya mfululizo wa kozi nne zitakazodumu kwa majuma mawili
kila moja, maofisa 88 ngazi za kati na juu kutoka kila mkoa katika
nchini watafunzwa na wakufunzi waandamizi nane kutoka katika Chuo cha
Mafunzo ya Polisi cha Uingereza,” amesema Hogan
Mgeni
Rasmi Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon
Sirro aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
SACP Simon Sirro akiteta jambo na Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka, UNDP, William Hogan baada ya picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment