KAMPUNI ya Proin Promotions Limited ambayo ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents inapenda kuutangazia Umma wa Watanzania na Wadau wote wa Tasnia ya Maigizo Tanzania kuwa imepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za msiba wa Mtayarishaji na Muongozaji mahiri wa Vipindi vya Runinga na Filamu,George Tyson.
Tyson alifariki dunia 30 Mei 2014 kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Gairo mkoani Morogoro akiwa njiani kurudi Dar es Salaam.
Ikumbukwe kuwa kabla ya taarifa hizo za msiba kupatikana shindano la
Ikumbukwe kuwa kabla ya taarifa hizo za msiba kupatikana shindano la
Tanzania Movie Talents lilikua linaendelea katika Kanda ya Pwani ambapo usaili ulianza tarehe
30 Mei 2014 saa mbili asubuhi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam.
Kutokana na msiba huu ambao pia umemgusa moja kwa moja mmoja wa majaji wetu katika Shindano hili
Kutokana na msiba huu ambao pia umemgusa moja kwa moja mmoja wa majaji wetu katika Shindano hili
Bi Vyonne Cherry (Monalisa)
ambaye marehemu alikuwa mzazi mwenzake na walibahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Sonia.
Tunapenda kuutangazia Umma na wadau wa Tansia ya Filamu Tanzania kuwa, Sisi Kama wadau wa Filamu Tanzania tumeamua kusitisha Usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents kwa Kanda ya Pwani mpaka pale msiba utakapomalizika.
Tunapenda kutoa pole kwa familia ya
Marehemu George Tyson kwa Jaji Wetu
Vyonne Cherry na kwa wadau wote wa Tasnia ya Filamu Tanzania.
Hakika tumempoteza mtu mahiri katika tasnia hii ya filamu na vipindi vya Televisheni.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amen
Hakika tumempoteza mtu mahiri katika tasnia hii ya filamu na vipindi vya Televisheni.
No comments:
Post a Comment